Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametangaza timu ya pili
ya Taifa (Young Taifa Stars) atakayoitumia kuangalia wachezaji ambao
baadaye anaweza kuwajumuisha kwenye timu ya wakubwa.
Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo (Aprili 23
mwaka huu) kabla ya kutaja kikosi hicho, Kim amesema timu hiyo ni sehemu
ya Mpango wa Maendeleo wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
uliozinduliwa Aprili 4 mwaka huu ukilenga kuendeleza wachezaji.
Amesema timu hiyo inajumuisha wachezaji ambao wamepita umri wa
kuchezea timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20
(Ngorongoro Heroes) na wakubwa ambao hawajapata fursa ya kuingia Taifa
Stars, lakini atatumia Young Taifa Stars kuangalia uwezo wao.
“Timu hii ni kiungo kati ya vijana na wakubwa. Wengi wa wachezaji
watakuwa vijana, lakini wakubwa wachache watapata fursa ya kuwemo ili
kuangalia uwezo wao hata kama uko nyuma waliwahi kuchezea Taifa Stars.
Lakini timu hii vilevile ni changamoto wa wachezaji wa Taifa Stars kuwa
wapo wanaosubiri wazembee ili wachukue nafasi zao,” amesema.
Young Taifa Stars yenye wachezaji 30 itakuwa na kambi ya siku tano jijini Dar es Salaam kuanzia Mei 2 hadi 6 mwaka huu.
-Chanzo TFF
Makipa | |
Aishi Manula | Azam |
Hussein Shariff | Mtibwa Sugar |
Ali Mustapha | Yanga |
Mabeki | |
Kessy Hassan | Mtibwa Sugar |
Kennan Ngoma | Barnsley FC, Uingereza |
Himid Mao | Azam |
Ismail Gambo | Azam |
David Mwantika | Azam |
Miraji Adam | Simba |
Mohamed Hussein | Kagera Sugar |
Waziri Salum | Azam |
Samih Nuhu | Azam |
Emily Mgeta | Simba |
Viungo | |
Haruna Chanongo | Simba |
Edward Christopher | Simba |
Mudathiri Yahya | Azam |
William Lucian | Simba |
Jonas Mkude | Simba |
Hassan Dilunga | Ruvu Shooting |
Jimmy Shoji | JKT Ruvu |
Abdallah Sesem | Simba |
Ramadhan Singano | Simba |
Farid Mussa | Azam |
Vicent Barnabas | Mtibwa Sugar |
Washambuliaji | |
Hussein Javu | Mtibwa Sugar |
Jerome Lambele | Ashanti United |
Zahoro Pazi | JKT Ruvu |
Twaha Hussein | Coastal Union |
Abdallah Karihe | Azam |
Juma Luizio | Mtibwa Sugar |
Post a Comment