KATEKISITA AINGIA MITINI KUOMBEA MAITI , MSELA AOKOA JAHAZI .....

 Kijana fundi  seremala ambae  pia alichonga  jeneza la marehemu Bw Solomon a.k.a Baba akiliweka wakifu kaburi kwa kulimwangia mchanga ambao  yeye alidai ni maji ya uzima
 Baadhi ya  waombolezaji  wa msiba  huo  wakiwa  wamekata tamaa baada ya katekista  kuingia mitini leo
 Hapa mhubiri  wa kujitolea  akiongoza ibada ya mazishi
 Mwili  wa marehemu Rejina Lweve  ukiwa makaburini









Baadhi  ya  waombolezaji  wa msiba  wa Bi Rejina  Lweve mkazi  wa  Kihesa katika Manispaa ya  Iringa wameeleza kusikitishwa kwao na udanganyifu uliofanywa na mmoja kati ya makatekista  wa RC eneo la Mgongo  baada ya mtumishi huyo  wa Mungu kudaiwa kutumia lugha ya udanganyifu  kukwepa kuongoza idaba ya mazishi kwa madai  kuwa anakwenda kutafuta maji ya uzima

Tukio  hilo  lilionyesha kuwakwaza  zaidi waombolezaji hao na kupelekea baadhi yao  kuamua kuondoka kabla ya shughuli za mazishi  kufanyika.

Wakizungumza na mtandao huu  wa www.francisgodwin.blogspot.com baadhi ya  waombolezaji  walisema  kuwa hawajapendezwa na hatua ya  kiongozi huyo  wa kidini  kususia  kuongoza  ibada  hiyo na  kuwa kufanya hivyo ni  kushusha  heshima la kanisa  hilo la RC ambalo  linaheshimika  zaidi duniani .

Hivyo  wamemwomba askofu wa kanisa  hilo mkoani Iringa  kulitazama kwa kina  suala  hilo ili ikiwezekana  kuwaondoa watendaji kazi wa parokia na vigango ambao  wanatabia kama  hizo za  kusisia maiti.

Pia  walisema kuwa kateksta  huyo aliaga  kuwa anakwenda kufuata maji ya uzima  nyumbani kwake ila toka alipoondoka mida ya saa 8 hakuweza kurejea tena hadi saa 10 jioni  walipoamua kumtuma dereva wa  boda boda  kumfuata  bila mafanikio na kulazimika kumwomba mchonga majeneza Kihesa ili  kuendesha idaba hiyo.

Post a Comment

Previous Post Next Post