LIBOLO WAIPIGA 4-2 JUMLA EL MERREIKH, WASONGA MBELE TENA


Recreativo de Libolo ya Angola, jana imefuzu kuingia Raundi ya Tatu ya Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya kuifunga El Merrekih ya Sudan mabao 2-1 mjini Khartoum. Matokeo hayo, yanamaanisha, Libolo imesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-2, baada ya kushinda pia 2-1 katika mchezo wa kwanza nyumbani Angola. Libolo iliingia Raundi ya Pili, baada ya kuitoa Simba SC ya Tanzania kwa jumla ya mabao 5-0, ikishinda 4-0 Angola na 1-0 Dar es Salaam. Timu hii inapewa nafasi ya kufika mbali katika michuano hii

Post a Comment

Previous Post Next Post