| Recreativo
de Libolo ya Angola, jana imefuzu kuingia Raundi ya Tatu ya Ligi ya
Mabingwa Afrika, baada ya kuifunga El Merrekih ya Sudan mabao 2-1 mjini
Khartoum. Matokeo hayo, yanamaanisha, Libolo imesonga mbele kwa ushindi
wa jumla wa mabao 4-2, baada ya kushinda pia 2-1 katika mchezo wa kwanza
nyumbani Angola. Libolo iliingia Raundi ya Pili, baada ya kuitoa Simba
SC ya Tanzania kwa jumla ya mabao 5-0, ikishinda 4-0 Angola na 1-0 Dar
es Salaam. Timu hii inapewa nafasi ya kufika mbali katika michuano hii |
إرسال تعليق