Na Bosire Boniface, Garissa
Wakati Kenya inaanza kujiondoa katika utawala wa serikali kuu,
magavana watatu kutoka kaskazini mashariki wanasema wanapanga kupunguza
mivutano miongoni mwa koo kwa kutumia sera sawa ya ajira kwa kazi za
utumishi wa umma.
"Serikali shirikishi ni muhimu katika kuondoa wimbi la vurugu za
kikabila ambazo zimezuia maendeleo katika mkoa huo," alisema Ali Ibrahim
Roba, gavana mpya mteule wa Kata ya Mandera.
Roba alisema atajaribu kubadilisha tabia iliyoshikiliwa muda mrefu
ambapo viongozi wa mkoa waliwapendelea watu wa koo zao kwa nafasi za
utumishi wa umma katika tawala zao. Zoezi kama hilo huwatenga watu
kutoka koo nyingine, jambo linalosababisha kuzuka kwa upinzani wa
vurugu, alisema.
"Sasa, tutaongozwa na katiba ambayo inaelezea kuwa jimbo linapaswa
kuzizingatia jamii zote na makundi mahsusi katika kuajiri na kugawana
rasilimali," aliiambia Sabahi, na kuelezea kuwa Kata ya Mandera ina koo
tatu kuu na kiasi cha koo saba ndogondogo.
Kupitia mchakato wa kuhamisha madaraka mikoani ulioainishwa katika katiba ya Kenya ya mwaka 2010, na kufanywa kuwa sheria na Sheria ya Uhamishaji Madaraka ya Serikali ya mwaka 2012, kata zitachukua nafasi ya majimbo kama kiungo cha serikali chini ya serikali ya taifa.
Utawala wa mkoa ambao huko nyuma ulijulikana kama Mkoa wa Kaskazini
Mashariki sasa umehamishwa katika Kata za Mandera, Wajir na Garissa ili
rasilimali kuwa karibu na wananchi badala ya kuwa mbali kutoka Nairobi.
Kata zitadhibiti fedha zao na zoezi la ajira kwa kazi za kiwango cha
ajira za umma, alisema Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mpito Kinuthia Wamwangi.
Bodi za Kata za Kazi za Umma (CPSB) zilianzishwa tarehe 28 Machi ili
kuchunguza na kuajiri wafanyakazi katika serikali 47 za kata tofauti.
CPSB zinachukua nafasi ya Tume ya Ajira ya Umma, ambayo ndiyo ilikuwa
dhamana ya serikali ya taifa kwa kuajiri watumishi wa umma, alisema.
Mfumo wa kiwango au unaotokana na sifa?
Viwango ambavyo kazi hugawiwa miongoni mwa koo kadhaa ni lazima kwa
sababu ya historia ya ushindani wa koo jimboni humo, alisema Gavana wa
Kata ya Garissa Adam Nathif Jama.
"Kugawa nafasi za kazi miongoni mwa koo hakuna maana kuwa kutaharisha
mfumo wa sifa. Koo na vikundi maalum vitapewa nafasi. Ikiwa [kazi]
inahusu sifa, kila ukoo na vikundi maalum vitakuwa na watu wao wenye
sifa miongoni mwa makundi yao," alisema.
Ingawaje yeye anaunga mkono mfumo wa viwango, Gavana wa Kata ya Wajir
Ahmed Abdullahi alisema kuwa itakuwa ngumu kutekeleza sera kama hiyo na
kuhakikisha kuwa kila ukoo au ukoo mdogo unapata mgao wa kazi za
serikali ya kata.
"Kuna kazi chache sana kwa kuhakikisha kuwa kila koo inapata sehemu
yake. Lakini ni bora zaidi hivyo kuliko utaratibu wa huru-kwa-wote kwa
sababu hilo linaweza kupelekea koo moja kuhodhi kila kitu. Jambo hili
litakuwa kama mbolea ya migongano, kwa vile wale watakaoachwa nje
wanaweza kuhujumu maendeleo yaliyopo," Abdullahi aliiambia Sabahi.
Hata hivyo, katika mfumo wa uhamishaji madaraka, zoezi la ajira kwa kazi za umma litakuwa la haki na la uwazi, alisema.
Viwango vinapaswa kutumika tu kama hatua za muda mfupi, alisema
Mkurugenzi Mtandaji wa WomanKind Kenya, Abdullahi Mohammed Abdi. Yeye
anapendelea sera ya ajira inayohamasisha watu kustahili kuwa na kazi
kutokana na sifa.
"Serikali ya kata itakuwa na mpito kutoka mfumo wa koo kwenda mfumo
wa sifa ambao kwa muda mrefu ili kuhamasisha ushindani na kiwango bora,"
alisema. "Katika hali nyingine, serikali za kata zitahatarisha sifa ili
kulifurahisha kabila, jambo ambalo Iitahatarisha matokeo."
إرسال تعليق