NDOLANGA AAPA KUANIKA UCHAFU WOTE WA TFF KWA FIFA

WAKATI ujumbe kutoka Shirikisho la Soka Dunia (FIFA) utatua nchini Aprili 16 kwa ajili ya kufanya tathmini ya mchakato wa uchaguzi, Mwenyekiti wa zamani wa Chama cha Soka Tanzania (FAT), Muhidin Ndolanga amesema atahakikisha anaanika madudu yote yaliyofanywa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Ndolanga aliyasema hayo jijini Dar es Salaam na kusisitiza kuwa sio yeye peke yake ambaye atakuwa mstari wa mbele kueleza madudu ya shirikisho hilo kwani wapo wengi.
"Mimi najua wapo watu wengi tu ambao wataenda kueleza yaliyotokea mpaka tukafika hapa tulipo, FIFA hawana wanachokijua watataka kujua ukweli kutoka kwetu, sisi kama wadau tutasema yetu na TFF nao watasema yao."alisema Ndolanga ambaye ni mjumbe wa heshima wa shirikisho hilo.
“Haiwezekani TFF ifanye madudu katika utendaji wake na bado itegemee watu wakae kimya. Yaani dhambi na dhuluma ziachwe hivihivi, ukiuliza Fifa, mara  Fifa watatufungia, mara fifa hivi, ...,” alisema Ndolanga ambaye enzi ya utawala wake kilichokuwa Chama cha Soka (FAT), Tanzania kiliwahi kufungiwa kwa sababu ya serikali kuingilia kati utendaji wake.
Wakati Ndolanga akisema hayo kuna habari kutoka kwa kiongozi mmoja mwenye wadhifa mkubwa TFF amebainisha kuwa mgombea wa nafasi ya urais Jamali Malinzi ana nafasi finyu ya kurejeshwa kwenye kinyang'anyiro hicho kwa kile walichoeleza kuwa amefanyiwa hujuma na klabu yake ya Yanga ambayo ilimuandikia barua ya kielelezo kuwa ameongoza Yanga kwa miaka miwili.
"Ni kweli kabla ajawa katibu wa Yanga alikuwa seneta na baadae katibu, lakini hakuna na kielelezo chochote ambacho kilionyesha zaidi ya barua ya katibu wa Yanga Laurance Mwalusako ambayo ilitanabaisha aliongoza Yanga miaka miwili.
"Alafu hata mkoa wa Pwani hakupeleka kielelezo kuwa anaongoza kamati ya mashindano wala mkoa wa Dar es Salaam vidhibitisho hiyo havikuwepo sasa kama Malinzi anaweza hakikishe anapata vielelezo hivyo vyote itakapokuja FIFA awe navyo." alisisitiza.

Post a Comment

Previous Post Next Post