Matairi yanachomwa katikati ya barabara |
Hii ndiyo hali halisi ya Mji mdogo wa Tunduma leo kuanzia asubuhi |
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Diwani akiongea na waandishi wa habari |
Wanafunzi wakisindikizwa na jeshi la polisi kurudi majumbani mwao |
Polisi wakiendelea kazi yao katika mitaa ya Tunduma |
Baadhi ya magati ya IT yaendayo nchini Zambia yakiwa yamepakiwa nnje kidogo ya mji wa Tunduma kuogopa kuharibiwa kwa magari hayo |
Diwani
wa kata ya Tunduma Ndugu Frank Mwaijoka (Chadema) pamoja na mchungaji
wa kanisa la KKT katika eneo hilo la Tunduma wilayani momba Mkoani mbeya
wametakiwa kujisalimisha kituo cha Polisi Tunduma mara baada ya
kuhusika na uchochezi wa kidini hali ambayo imepelekea kutokea kwa
vurugu katika eneo hilo.
Vurugu
hizo zimeanza majira ya saa 3:asubuhi katika eneo hilo la tunduma mara
baada ya kundi la watu wanaodai kuwa wao ni wafuasi wa dini ya kikristo
wakidai waruhusiwe kuchinja mifugo na kuuza katika mabucha yao hali
iliyo pelekea kuibuka kwa vurugu hizo.
Akizungumza
kuhusiana na tukio hilko Kamanda wa Polisi Mkoani humo Ndugu Diwani
Athumani amesema kuwa kufuatia kuwepo kwa tukio hilo jumla ya watu zaidi
ya 40 tayari wamekwisha kamatwa .
Amesema
mpaka sasa taarifa walizo zipata kufuatia vurugu hizo zinaeleza kuwa
miongoni mwa watu walichochea vurugu hizo ni diwani wa kata hiyo ya
Tunduma Ndugu John mwaijoka pamoja na Mchungaji wa kanisa la kkt ndugu
Neema Mwaipusa ambao kwa pamoja wametakiwa kujisalimisha kituo cha
polisi kwa mahojiano zaidi.
Amesema
suala hilo limegubikwa na siasa kwani tayari viongozi wa serikali
akiwemo Mkuu wa mkoa huo Ndugu Abbas Kandoro amekwisha litolea ufafanuzi
Apri 02 mwaka huu wakiwepo pia viongozi wa dini .
Amesema
kwa asilimia kubwa mgogoro huo juu ya nani achinje umeingiliwa na mambo
ya kisiasa kwani hata baadhi ya wananchi wa maeneo hayo wamekuwa
wakilalamika juu ya kutokea kwa vurugu hizo.
Amesema
shughuli za kibiashara katika eneo hilo zimeshindwa kufanyika katika
eneo hilo hivyo kufanya wananchi kupata adha hasa kwa nchi jirani ya
Zambia ambao kwa asilimia kubwa wanategema kupata mahitaji kutoka
mpakani mwa Tanzania.
Hata
hivyo Diwani amesema kuwa katika vurugu hizo askari mmoja pamoja na
mwananchi wamejeruhiwa kwa kupigwa mawe ambapo tayari wamekwisha
fikishwa kituo cha polisi.
Kufuati
hali hiyo Kamanda huyo wa Polisi amesema kwa sasa hali imelejea katika
hali yake ya kawaida hivyo amewataka wananchi wa maeneo hayo kuwa
watulivu wakati jeshi hiulo la Polisi likiendela na msako wa kuwatafuta
wahalifu wengine.
Picha na Mbeya yetu
|
إرسال تعليق