Kituo
cha televisheni cha SuperSport cha Afrika Kusini kitaonesha moja kwa moja mechi
sita za Ligi Kuu ya Vodacom katika Super Week kati ya Aprili 11 na Mei 18 mwaka
huu.
Mechi
hizo ni kati Azam na African Lyon itakayochezwa Aprili 11 mwaka huu badala ya Aprili
10 mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam.
Yanga
na Oljoro JKT ambayo sasa itachezwa Aprili 13 mwaka huu badala ya Aprili 10
mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Azam
na Simba itakayochezwa Aprili 14 mwaka huu badala ya Aprili 13 mwaka huu Uwanja
wa Taifa, na mechi kati ya Coastal Union na JKT Ruvu itakayochezwa Aprili 16
mwaka huu badala ya Aprili 10 mwaka huu.
Mechi
nyingine ya Super Week itakayochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga ni kati
ya Mgambo Shooting na Yanga itakayofanyika Aprili 17 mwaka huu badala ya Aprili
13 mwaka huu.
Pia
mechi nyingine itakayooneshwa live na SuperSport ni kati ya Yanga na Simba
itakayofanyika Mei 18 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kutokana
na mechi za Super Week, mechi kati ya Mtibwa Sugar na Oljoro JKT iliyokuwa
ichezwe Aprili 13 mwaka huu sasa itachezwa Aprili 17 mwaka huu Uwanja wa
Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
Boniface
Wambura
Ofisa
Habari
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

إرسال تعليق