Taarifa za habari: Mwanachuo DSJ afariki ajalini; Bajeti W/Maji yapita

Picture

Hili ni gari lililopata ajali maeneo ya Chalinze mkoa wa Pwani jana usiku lenye namba za usajili T150 BJR Toyota Coaster ililokuwa limebeba wanafunzi wa chuo cha Uandishi wa Habari (DSJ) wakitokea katika ziara ya kimasomo mkoani Mbeya (Imma Matukio blog)


Watu wawili ambao wametajwa kuwa ni Mwanafunzi na Waziri katika Chuo cha Uandishi wa Habari cha Dar es Salaam (DSJ) na dereva wa gari walimokuwa wamepanda, wamepoteza maisha katika ajali iliyotokea usiku wa leo katika barabara kuu ya Morogoro-Iringa.


Ajali hiyo iliyowaacha watu 22 wakiwa na majeraha, ilitokea baada ya gari walimokuwemo lenye namba za usajili T 150 BJR aina ya Toyota Coaster likiendeshwa na dereva Ally Kinyasi likitokea Mbeya, kugongana uso kwa uso na lori la mafuta lililokuwa lilokuwa linaendeshwa na dereva Mbwana Hassan kutokea Dar es Salaam.

Kamanda wa Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Pwani, Nassor Sisiwaya alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kumtaja marehemu mwanachuo huyo kuwa ni  Deo Kibona.

Alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari namba wa gari la abiria kujaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake ya uangalifu na hivyo kusababisha kuvaana uso kwa uso kwa uso na lori.

Bofya kifute cha pleya ya WAPO radio FM iliyopachikwa hapo chini, ili kusikiliza zaidi kuhusu taarifa hii na nyinginezo.




Baada ya kuahirishwa wiki ijayo, hatimaye leo Serikali imetangaza kuwa imekubali kutenga shilingi bilioni 184.5 kwenye bajeti ya Wizara ya Maji kwa mwaka wa fedha 2013/2014, kama ilivyopendekezwa na Kamati ya kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji na Wabunge wengi waliochangia.

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amewataka viongozi wa vyama vya siasa, jumuiya na taasisi mbalimbali kuwaachia wananchi uhuru wao wa kutoa maoni kuhusu upatikanaji wa Katiba Mpya. 

Taarifa hizo na nyinginezo zinasikika katika pleya za habari zilizopachikwa hapo chini



Post a Comment

Previous Post Next Post