TAMKO LA SERIKALI KUHUSU UHAMAJI KUTOKA MFUMO WA UTANGAZAJI WA ANALOJIA KWENDA DIJITALI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

TAMKO LA SERIKALI KUHUSU UHAMAJI KUTOKA MFUMO WA
UTANGAZAJI WA ANALOJIA KWENDA DIJITALI

Mabadiliko katika mfumo wa utangazaji kutoka mfumo wa analojiakwenda katika mfumo wa dijitali ni utaratibu ambao unaendeleaulimwenguni kote. Mabadiliko haya yanatokana na makubaliano ya nchiwanachama wa Shirika la Umoja wa Mataifa lenye dhamana ya masualaya mawasiliano yaani
International Telecommucations Union
yaliyofanyika mwaka 2005 huko Geneva, Uswisi. Makubaliano ya nchiwanachama ni kuzima kabisa matangazo katika mfumo wa analojia nakutumia mfumo wa utangazaji wa dijitali ifikapo tarehe 17 Juni 2015.Ili kuhakikisha mabadiliko haya yanafanyika kwa ufanisi, tija na piakutoa muda wa kutosha wa kutekeleza mabadiliko haya, mwaka 2005Serikali ilianza mchakato wa uhamaji kutoka mfumo wa utangazaji waanalojia kwenda dijitali ambao ulihusisha wadau wote, wakiwemowamiliki wa vyombo vya habari na vituo vya utangazaji wa televisheni,hatua kwa hatua, hadi kuridhia ratiba nzima ya uzimaji wa mitambo yaanalojia. Kwa kifupi mchakato wa uhamaji ulipitia hatua zifuatazo:
Mwaka 2005
:Waraka wa kwanza wa mashauriano (consultativedocument) kuhusu umuhimu na faida za kuhama kutokamfumo wa utangazaji wa analojia kwenda dijitaliulitayarishwa na kusambazwa kwa wadau wote;
Mwaka 2006:
Waraka wa pili wa mashauriano na mapendekezo yamuundo wa leseni kwenye mfumo wa utangazaji wateknolojia ya dijitali ulitayarishwa na kusambazwa kwawadau wote;
Mwaka 2007:
Kamati ya kiufundi inayoshughulikia uhamaji kutokamfumo wa utangazaji wa analojia kwenda dijitaliiliundwa;
1


Mwaka 2007:
Mkutano mkuu uliojumuisha vituo vyote vya utangazajinchini ulifanyika Bagamoyo kupitisha maazimio yamfumo wa leseni za utangazaji utakaotumika kwenyemfumo wa dijitali;
Mwaka 2010:
Kampuni tatu (3) zilipewa leseni za ujenzi wamiundombinu ya utangazaji ya dijitali. Kampuni tatuzilizopewa leseni za kusambaza matangazo ya dijitali niAgape Associates Limited, Basic Transmission Limited,na Star Media (T) Limited. Kampuni hizo zilipewa lesenibaada ya kuthibitisha kuwa zina uwezo wa kujengamiundombinu ya kurushia matangazo katika mfumo wadijitali;
Mwaka 2010
:Kamati ya Kitaifa ya Kuratibu Mabadiliko ya Utangazajitoka mfumo wa analojia kwenda dijitali iliundwa.Kamati hii hukutana kila baada ya miezi mitatukutathmini maendeleo ya ubadilishaji wa mfumo wautangazaji;
Mwaka 2011
:Kampeni ya Kitaifa ya kuelimisha umma kuhusumabadiliko ya mfumo wa utangazaji ilizinduliwa rasmina Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania.Ili kuhakikisha kuwa ujenzi wa miundombinu ya urushaji wa matangazokatika mfumo wa dijitali unaendana na ratiba ya uhamiaji katikamfumo wa matangazo kutoka mfumo wa analojia kwenda dijitali,taarifa za mara kwa mara zimekuwa zikiletwa na wajenzi wamiundombinu hiyo katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania nakujadiliwa na Kamati mbalimbali zinazohusiana na masuala ya uhamajikatika mfumo wa utangazaji wa dijitali. Taarifa hizo zimekuwazikionyesha kuwa ujenzi wa miundombinu unaendelea vizuri nakwamba ratiba ya uzimaji wa mitambo ya analojia nchini itakwendakama ilivyokubalika na wadau wa utangazaji.Kufuatia uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Kuelimisha umma kuhusumabadiliko ya mfumo wa utangazaji kutoka katika mfumo wa analojiana kwenda katika mfumo wa dijitali uliofanywa na Mhe. Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali, kwa kupitia Mamlaka yaMawasiliano Tanzania, iliandaa
Mkakati Maalum wa Mawasiliano
ambao ulilenga katika kuhamasisha wananchi kuhusu uhamaji katikamfumo wa utangazaji wa dijitali. Njia mbalimbali zimetumika katikakuelimisha umma kuhusu mabadiliko ya mfumo wa utangazaji ikiwa nipamoja na kufanya mikutano ya hadhara sehemu mbalimbali, kutoa
2

vipeperushi na matangazo katika magazeti, redio na televisheni,kufanya majadiliano katika televisheni na redio ambayo yalihusisha piamaswali kutoka kwa wadau mbalimbali, kuweka taarifa katika tovutikuhusu masuala mbalimbali ya uhamaji katika mfumo wa utangazaji.Taarifa zilizopo zinaonyesha kuwa uhamasishaji na elimu kwa ummaimetolewa kwa kiasi kikubwa na wananchi wamehamasika sana katikakuingia katika mfumo wa utangazaji wa dijitali kutoka ule wa analojia.Hii ni kutokana na wananchi wengi kujitokeza kununua ving’amuzi(visimbuzi) kwa wingi katika Jiji la Dar es Salaam na maeneo mengineambayo matangazo katika mfumo wa analojia yalitarajiwa kuzimwa.Aidha,
hapakuwa na mapendekezo yoyote kutoka kwa wajenzi wamiundombinu ya urushaji wa matangazo ya dijitali
kuwawatashindwa kujenga miundombinu hiyo kwa wakati ifikapo tarehe 31Desemba 2012, siku ambayo ilikuwa imekubalika kuzima mitambo yautangazaji ya mfumo wa analojia na kuanza kutumia mfumo wadijitali. Tarehe 31 Desemba 2012, Serikali ilianza kuzima matangazohayo kwa awamu ili kubaini na kushughulikia changamoto mbalimbaliambazo zingeweza kujitokeza katika mabadiliko hayo.Uzimaji wa mitambo ya utangazaji wa analojia kwenda katika mfumowa utangazaji wa dijitali ilianza kutekelezwa tarehe 31 Desemba 2012kwa kuzima mitambo 14 ya televisheni inayotumia utangazaji wamfumo wa analojia katika jiji la Dar es Salaam ambapo wananchi wengiwalinunua ving’amuzi ili waweze kujiunga na mfumo mpya wautangazaji wa dijitali. Kadhalika, uzimaji wa mitambo ya analojiakwenye miji ya Dodoma na Tanga ulifanyika tarehe 31 Januari 2013.Uzimaji wa mitambo ya analojia kwa jiji la Mwanza ulifanyika tarehe28 Februari 2013. Uzimaji wa mitambo kwa miji ya Arusha na Moshiumefanywa tarehe 31 Machi 2013. Kwa ujumla wananchi wamekuwawakijitokeza kwa wingi kujiunga na mfumo huu mpya wa utangazaji nahakuna matatizo yaliyojitokeza zaidi ya changamoto kadhaa ambazozimeendelea kupatiwa ufumbuzi.Ikumbukwe kuwa uzimaji wa urushaji wa matangazo katika mfumo waanalojia na kuanza kutumika kwa mfumo wa dijitali umefanywa mahaliambapo kuna mawimbi (signal) ya televisheni ya dijitali tu. Paleambapo hakuna mawimbi ya televisheni ya dijitali, matangazo yatelevisheni yameendelea kurushwa katika mfumo wa analojia hadiwakati ambapo mawimbi ya televisheni ya dijitali yatakapofikia mahali
3
Zaidi  Bofya hapa

Post a Comment

أحدث أقدم