
Mhandisi wa Kampuni ya Dr Gogo engineering limited, Godwin Kalaghe (kulia), akimkabidhi Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo nyaraka za taarifa za kukamilika kwa ujenzi wa kisima cha maji katika Kijiji cha Makanya, wilayani Same juzi. Ujenzi wa kisima hicho uliogharimu sh. mil. 51.6 ulifadhiliwa na TBL.

Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),
Steve Kilindo akisaidia kumtwisha ndoo ya maji mkazi wa Kijiji cha
Makanya, wilayani Same, Asia Zuberi ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mradi
wa kisima cha maji kwa msaada wa TBL kwa gharama ya sh. mil. 51.6.
Hafla hiyo ilifanyika kijijini hapo juzi.

Mradi wa kisima cha maji kilichofadhiliwa na kampuni ya bia Tanzania
katika kijiji cha Makanya wilayani Same chenye thamani ya shilingi
milioni 51.6.Uwepo wa kisima hiki utasaidia kupunguza tatizo la maji
hususani kwa wakazi wa Tambarare katika wilaya ya Same.
hususani kwa wakazi wa Tambarare katika wilaya ya Same.
إرسال تعليق