Diwani wa kata ya Bulyanhulu Bw. Joseph Makoba akikata utepe kuzindua minara mipya ya kampuni ya simu za mkononi Tigo kata za Kakola na Segese wilayani Kahama mkoani Shinyanga, anayeshuhudia ni meneja wa Tigo kanda ya Ziwa Bw.Joseph Mutalemwa.
Tigo Tanzania leo wanaendeleza mipango yao ya kuwekeza katika upanuzi wa mtandao wake katika Kata za Kakola na Segese wilayani Kahama Mkoani Shinyanga ili kuongeza kiwango cha ubora na upatikanaji wa mtandao huo nchini kote. Upanuzi huo pia utakwenda sambamba na kujenga miundombinu mipya ya mawasiliano hasa katika maeneo ya vijijini, kuleta mawasiliano kwa maelfu ya watu. Minara mipya ya mawasiliano itajengwa nchi nzima ambapo mradi huo umeanzia katika mkoa wa Kigoma na kuendelea maeneo kama Mwanza, Tabora, Mara na Kagera.
Akitangaza mradi huo, Meneja Mkuu wa Tigo Bw. Diego Gutierrez alisema “Tigo Tanzania imeendelea kukua kwa kasi mwaka hadi mwaka. Bidhaa zetu za kipekee na huduma pamoja na kuongezeka kwa wateja ni ushahidi wa wazi kabisa wa kukua kwetu. Uzinduzi wa minara hii mipya utawezesha kuwapatia wateja wetu bidhaa bora za kipekee zilizobuniwa katika ubora wa hali ya juu ili wateja wetu waweze kunufaika na huduma na bidhaa zenye kiwango cha hali ya juu kabisa kwa hatua mpya. Hii ndio dhamira yetu ambayo imetufanya tuendelee kuwa kampuni inayoongoza ya mtandao wa simu za mkononi Tanzania.”
Tukiwa tayari na mtandao imara wa mawasiliano katika mikoa mingi ya Tanzania bara na Zanzibar, upanuzi huu wa mtandao wetu unalenga kuhakikisha kuwa mtandao wetu unapatikana katika mikoa mingi zaidi nchini. Itaboresha ubora wa mtandao katika maeneo ambayo tayari yana mtandao wa Tigo kuhakikisha mawasiliano yanaboreka zaidi na huduma za Intaneti zinapatikana vizuri zaidi na wakati huo huo kuhakikisha kuwa tunapeleka huduma za mtandao wa Tigo nje kidogo ya Tanzania, kuwawezesha wateja wapya kuungana na wenzao ulimwenguni na kuwa sehemu ya jamii kubwa ya mtandao wa mawasiliano ya simu.
“Tukiwa tunajiamini katika utoaji wa huduma bora za mawasiliano ya simu na nia ya kuendelea kusonga mbele zaidi kwa siku zijazo, tumeona umuhimu wa kupanua na kuboresha mtandao wetu. Uzinduzi wa minara hii mipya utatuwezesha kupanua huduma zetu za mawasiliano katika maeneo haya mapya, kwa wateja tulionao na tutakaokuwa nao kama tunavyodhamiria”
Awali upanuzi wa mtandao wa Tigo vijijini ulianzia kata za wilayani Kasulu mkoani Kigoma
Katika ripoti ya hivi karibuni ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ya robo mwaka ya mawasiliano ya mwezi Septemba 2012, idadi ya wateja wa Tigo iliongezeka kwa 20% kati ya mwezi Juni mwishoni 2012 na Septemba 30, 2012 ikiwa na wateja 630,000 walioripotiwa. Tukiwa na mikakati hii ya upanuzi, tunatarajia kukua zaidi kwa mwaka huu 2013.
إرسال تعليق