


…………………………………………………………………………
TTCL, imezindua huduma mpya ya Bando Na TTCL inayoambatana na punguzo
kubwa la bei kwa huduma ya INTERNET. Mtakumbuka ni Juzi tu tareha 21
Machi 2013 tulifungua kituo chetu kipya cha huduma kwa wateja
kilichopo Kariakoo katika mkoa wa Dar es Salaam katika kupanua mtandao wa huduma kwa wateja nchini (>30 CSC network nchini).
Kifuatacho sasa ni kupanua wigo wa huduma kwa wateja.
Vilevile mtakumbuka kuwa baada ya kujitambulisha sokoni na huduma ya
‘Mobile Internet’ isiyo na kikomo ya BANJUKA; kampuni ya simu ya TTCL
sasa inazindua huduma mpya inayojulikana kama ‘BANDO NA
TTCL’. Huduma hii inamuwezesha mteja kufaidika na meseji za bila
kikomo, kuperuzi intaneti na muda wa maongezi kwenda mitandao yote kwa
wakati mmoja kwa bei hadi ya shilingi 500. BANDO NA
TTCL inawalenga zaidi watumiaji wa simu za kisasa za smart phones za
TTCL (zinazopatikana ktk vituo vya huduma kwa wateja nchini).
Maelezo zaidi ya juu ya
huduma hii yanapatikana kwa kupiga 100 huduma kwa wateja au tembelea
ofisi zetu za mauzo zilizoenea nchi nzima. Aidha, TTCL
imeshusha kwa kiwango kikubwa bei ya vifurushi vyake vya mobile internet
kwa kampeni ya BASTI ikimaanisha peruzi intaneti zaidi kwa gharama
nafuu. Hili ni punguzo la bei la aina yake. Mathalani;
kifurushi cha mwezi cha 4GB kilichokuwa kinauzwa shilingi 90,000 sasa
kinauzwa kwa shilingi 25,000 tu. Hii ni nafasi si tu kwa wateja waliopo
wa TTCL kuongeza matumizi kwa gharama nafuu bali hata
kwa wateja wapya ikiwamo watumiaji wadogo kujiunga na mtandao wa TTCL.
(Haki ya mawasiliano kwa wote)
Leo hii, wateja wengi zaidi na hasa wanafunzi na wajasiliamali wanatumia simu za kisasa (smart phones, tablet PCs kama iPad, Samsung Galaxy nk) na kompyuta ili kupata huduma za intaneti na mitandao ya kijamii kwa mfano, Michuzi blog, facebook twitter, LinkedIn n.k ) kwa shughuli zao za kila siku. Upatikanaji wa vifaa hivi vya kisasa (sambamba na ukuaji wa teknolojia) na kumewezesha kukua kwa kasi kwa tabaka la kati lawatumiaji hivyo kumesababisha kukua maradufu kwa soko la intaneti hapa nchini. (Hili nijambo jema sana kwa nchi yetu na maendeleo ya watu wake kiuchumi na kijamii)
Kwa kuzingatia haya (na kutambua kuwa mawasiliano na habari ni swala mtambuka), TTCL ina
mikakati wa kuwawezesha wananchi wengi zaidi kupata huduma za intaneti
na mawasiliano & habari kwa ujumla na hivyo kuwa chachu kubwa ya
maendeleo nchini. Huduma mpya ya BANDO NA TTCL na kampeni ya BASTI ni juhudi za makusudi za TTCL katika kutimiza adhma hii.
Kwa kifupi huduma za BANDO NA TTCL na kampeni ya BASTI zina manufaa yafuatayo kwa mteja:
1. Huduma ya ‘mobile internet’ kwa gharama nafuu
2. Vifurushi vya siku, wiki na mwezi kulingana na mahitaji yako
3. ‘Mobile Internet’ yenye ubora na kasi ya juu zaidi
4. Kwa kununua modemu ya shilingi 29,900 utapata 2GB bure kuperuzi intaneti
5. Huduma ya BANDO NA TTCL inapatikana pia kwa simu za kisasa za smart phones.
6. Inakupa thamani bora kwa pesa yako
TTCL kama kampuni kongwe na mhimili wa mawasiliano nchini inatambua kuwa inalo jukumu
kubwa la kutoa huduma za mwasiliano kwa wateja wake nchini na nje ya
mipaka yake. Uwepo wa mitandao ya mawasiliano ya baharini ya EASSy na
SEACOM katika pwani ya Tanzania, mkongo wa Taifa wa
mawasiliano na mtandao wake ulionenea nchi nzima umeiwezesha TTCL kuwa
mstari wa mbele kutoa huduma za mawasiliano ikiwamo intaneti kwa ofisi
za serikali na benki mbalimbali hapa nchini. Mkongo wa Taifa umesaidia kuwa na huduma bora zaidi ambapo
kwa sasa wananchi tunaweza kupata huduma nyingi zikiwemo matibabu
mtandao, elimu mtandao, biashara mtandao na Serikali mtandao, Benki –
Mtandao, Pesa – mtandao na pia kufanikiwa kuifikisha Tanzania katika nchi za Zambia, Burundi, Rwanda na Malawi kwa huduma za mawasiliano.
TTCL itaendelea kupanua
wigo wa mtandao na huduma zake kukidhi mahitaji ya mawasiliano na habari
ya wateja wake na watanzania wote. Nisisitize tena
BANDO NA TTCL pamoja na BASTI imetengenezwa kukidhi mahitaji ya
watumiaji wote :- Maofisini, Biashara ,Vyuoni, mashuleni na pia
majumbani kwa familia.
Huduma ya BANDO NA TTCL
inakuwezesha kupata mgezi, kutuma meseji bila kikomo na kuperuzi –
Intaneti kupitia simu za mkononi. Kampeni ya BASTI inakupatia punguzo
kubwa la bei ya Mobile Intaneti kupitia modemu
zinazotumia teknologoia ya kisasa EVDO itolewayo na TTCL. Tumia huduma
hizi hakika utafurahia
إرسال تعليق