Waajiriwa wapya serikalini watakiwa kujua sheria, kanuni na taratibu zinazoendesha utumishi wa umma.

Katibu Mkuu wa wizara ya  Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda akifungua mafunzo elekezi ya siku mbili kwa watumishi wapya wa wizara hiyo leo katika ukumbi wa mikutano uliopo uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2012/13 imeajiri  watumishi wapya 30.
Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni kutoka wizara ya  Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Herman Mwasoko akiongea jambo wakati wa ufunguzi wa  mafunzo elekezi ya siku mbili kwa watumishi wapya wa wizara hiyo yaliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano uliopo uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala Enely Mwakyoma  na kushoto ni Mkurugenzi wa Michezo Leonard Thadeo. 
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Barnabas Ndunguru akitoa maelezo kuhusu mafunzo elekezi kwa watumishi wapya walioajiriwa na wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2012/13 leo katika ukumbi wa mikutano uliopo uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango Gasper Mwembezi.
Baadhi wa waajiriwa wapya kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakimsikiliza katibu Mkuu wa wizara hiyo Sethi Kamuhanda (hayupo pichani) wakati wa  ufunguzi wa mafunzo elekezi yaliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano uliopo uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya wakurugenzi kutoka  wizara ya  Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakimsikiliza katibu mkuu wa wizara hiyo Sethi Kamuhanda (hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo elekezi ya siku mbili kwa watumishi wapya wa wizara hiyo leo katika ukumbi wa mikutano uliopo uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) Assah Mwambene.
 Katibu Mkuu wa wizara ya  Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda akiongea jambo leo na  watumishi wapya wa wizara hiyo wakati wa mafunzo elekezi yanayofanyika  katika ukumbi wa mikutano uliopo uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2012/13 imeajiri  watumishi wapya 30 ambao wengi wao ni vijana.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Barnabas Ndunguru (kulia) akimwambia jambo Katibu Mkuu wa wizara hiyo Sethi Kamuhanda mara baada ya kumalizika kwa ufunguzi wa mafunzo elekezi kwa watumishi wapya leo katika ukumbi wa mikutano uliopo uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. 
Waajiriwa wapya kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, wakurugenzi wa Idara  na Baadhi ya wafanyakazi wa wizara hiyo wakiwa katika picha ya pamoja  mara baada ya kumalizika kwa ufunguzi wa mafunzo elekezi leo uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam . Watatu kushoto mstari wa mbele ni katibu Mkuu wa wizara hiyo Sethi Kamuhanda. (Picha na Anna Nkinda – Maelezo).
Na Anna Nkinda.  
Watumishi wa Umma wametakiwa kufanya kazi zao kwa uadilifu, bidii na kujituma huku wakifuata maadili ya kazi zao kwa kufanya hivyo wataweza  kutekeleza malengo ya Serikali ya kuwahudumia wananchi kama wanavyotarajia kupata huduma nzuri.
Wito huo umetolewa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya  Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo  Sethi Kamuhanda, wakati akifungua mafunzo elekezi ya siku mbili kwa wafanyakazi wapya yanayofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kamuhanda  amesema kuwa uvumilivu unatakiwa mahali popote pa kazi na lazima watumishi hao wawe na uwezo wa kukabiliana na changamoto watakazokutana nazo  kwa kufanya kazi kwa bidii na kujituma na siyo kukata tama, kwani mtu akifanya kazi kwa bidii viongozi wake wataiona kazi anayoifanya  na kumuhitaji mara kwa mara.
Aidha Kamuhanda amesema kuwa mtumishi wa sekta ya umma anafanya kazi ya kuwatumikia wananchi bila ya kubagua wala kupendelea hivyo basi hapaswi kuchagua kituo cha kufanyia kazi kwa kuwa hata wananchi walioko nje ya miji wanatakiwa kupata huduma sawa na wananchi wa mijini.
Kamuhanda amesema msiwe na tabia ya kuchagua maeneo ya kufanyia kazi kwani mtumishi wa umma anapangiwa kazi na mwajiri wake katika kituo chochote kile na huko mikoani ambako watumishi wengi hawapendi kwenda ndiko ambako utajifunza mambo mengi zaidi na kuweza kukabiliana na changamoto za kazi.
Katibu Mkuu huyo pia amewasihi wafanyakazi hao kuwa  na tabia ya kujifunza kutoka kwa watumishi waliowakuta kazini wenye uzoefu wa kazi na kutojifanya wajuaji  kwani  kwa kufanya hivyo watajiongezea  ujuzi wa kazi na  kufika mbali zaidi.
Akitoa maelekezo kuhusiana na mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Barnabas Ndunguru amesema kuwa waajiriwa  wapya wanatakiwa kujua sheria, kanuni na taratibu zinazoendesha utumishi wa umma.
Ndunguru amesema, “Mafunzo elekezi kwa watumishi wapya Serikalini yanawawezesha  kupata ufahamu wa mambo mbalimbali kupitia mada zitakazofundishwa ambazo baadhi yake ni majukumu ya wizara, maadili katika mtumishi wa umma, wajibu wa kupiga  vita rushwa mahali pa kazi na huduma kwa mteja”.
Alimalizia kwa kusema kuwa mafunzo elekezi  yatawawezesha watumishi hao kujitambua kuwa wao ni watumishi wa umma na kwamba wanatakiwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma na yataimarisha mahusiano kiutendaji kati ya watumishi wapya, wakuu wa Idara na vitengo vyote na watumishi wote wa wizara.
Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2012/13 imeweza kuajiri watumishi wapya 30 ambao wengi wao ni vijana kutoka kada mbalimbali.

Post a Comment

أحدث أقدم