Mheshimiwa
Angellah Kairuki(MB),Naibu Waziri wa Katiba na Sheria akiwa namwenyeji
wake Mhe.Sayid Ashraful Islam, Waziri wa Serikali za Mitaa Maendeleo
Vijijini na Ushirika(Wizara inayoshughulika na Usajili wa Vizazi
naVifo)wakati wa ziara yake nchini Bangladesh kujifunza namna ambavyo
nchi hiyo imewezakufikiaa silimia zaidi ya 95 ya usajili wa Vizazi
naVifo.

Mheshimiwa Angellah Kairuki, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari wa Bangladesh

Mheshimiwa Angellah Kairuki akifafanua jambo kwa Mhe.Mhe.
Hassanul Haq Inu, Waziri wa Habari wa Bangladesh wakati wawili hao
walipokuwa wakisubiri kukutana na waandishi wa habari wa Bangladesh na
kueleza madhumuni ya ujumbe wa Tanzania kwenda nchini Bangladesh
kujifunza namna ya kuboresha mfumo wa usajili wa vizazi na vifo hadi
kufikia asilimia mia moja (100%).

Mhe. Angellah Kairuki akielezwa jambo na Bw. Nazrul Islam, Mtendaji Mkuu wa Dhaka South City Corporation

Mhe.
Angellah Kairuki katika picha ya pamo jana Sir. Fazle Abed, Mwanzilishi
na Mwenyekiti wa taasisi ya BRAC alipotembelea Makao Makuu ya BRAC.

Mhe.
Angellah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wake wa
wataalam kutoka Taasisiza RITA, NIDA, TRA, Serikali zaMitaa,
e-Government, Tumeya Taifaya Uchaguzina Ofisi ya Takwimu Ofisi ya
Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Wenyeji wake.
----
USAJILI WA VIZAZI NA VIFO NCHINI
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mheshimiwa Angellah Kairuki aliongoza ujumbe wa Tanzania kwenda nchini Bangladesh tarehe 5-11 Aprili 2013.
Ujumbe huo uliojumuisha wataalam kutoka taasisi mbalimbali za Serikali zinazojihusihana masuala ya usajili ikiwa ni pamoja na RITA, NIDA, TRA, Serikali za Mitaa, e-Government,
Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Ofisi ya Takwimu ulikwenda kujifunza
namna ambavyo nchi ya Bangladesh ilivyoweza kufanikiwa katika zoezi la
Usajili wa Vizazi naVifo kwa zaidi ya asilimia 95 ya wananchi wao.
Katika
ziara hiyo Mheshimiwa Naibu Waziri na ujumbe wake walijionea jinsi
ambavyo zaidi ya huduma 16 muhimu nchini Bangladesh zilivyounganishwa na
Mfumo wa kusajili vizazi na vifo na umuhimu wa cheti cha kuzaliwa.
Huduma
hizo ni pamoja naVitambulisho vya Taifa, Leseni ya Biashara,
Kitambulisho cha mlipa Kodi (TIN), leseni ya kuendesh agari, hati ya
kusafiria, leseni ya ukandarasi, vibali vya ujenzi, leseni ya
kusafirisha na kuagiza bidhaa ndani na nje ya nchi, kuunganishi wa
huduma muhimu kama umeme, maji, simu n.k. bila kuwa na cheti cha
kuzaliwa mwananchi wa Bangladesh hawezi kupata huduma moja wapo kati ya
hizo.
Serikali
kwa kutambua umuhimu na faida za kusajili vizazi na vifo,imedhamiria
kuboresha mfumo wa Usajili na kunyanyua kiwango cha Usajili kwa
kuanzisha Mpango wa Usajili wa Watoto wote walio na umri chini yaMiaka
Mitano (Under Five Birth Registration Initiative(U5BRI) na mpango wa
usajili wa watoto wenye umri wa miaka 6-18.
Katika
mpango huu waUsajili,mtoto atasajiliwa na kupatiwa cheti papohapo, na
hivyo kufanya zoezi zima la usajili kuwa la hatua moja badala ya hatua
mbili zinazotumika sasa, yaani kusajili kwanza kisha kupata cheti
baadaye. Pia Mpango huu unalengo la kugatua madaraka ya shughuli za
usajili kutoa Serikali Kuu na kupeleka katika Serikali za Mitaa na Vituo
vya Afya.
إرسال تعليق