
Katibu
Mkuu wa Baraza la Wazee wa klabu ya Yanga mzee Ibrahim Akilamli
(katikati) akiongea na wandishi wa habari makao makuu ya klabu leo
Kuelekea
mchezo dhidi ya Simba SC mei 18, Baraza wa wazee wa klabu ya Young
Africans limeomba mwamuzi wa mchezo huo achezeshe kwa kufuata sheria 17
zote za mchezo na kwa kufanya hivyo mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya
Vodacom watoto wa Jangwani lazima wataibuka na ushindi katika mchezo
huo.
Akiongea
na wandishi wa habari kwa niaba ya baraza la wazee makao makuu ya
klabu, katibu mkuu wa baraza la wazee Mzee Ibrahim Akilimali
(Ibrahimovich) amesema wanaamini kikosi cha Yangaa kitaibuka na ushindi
katika mchezo huo ikiwa mwamuzi atachezesha kwa kufuata sheria zote 17
na kanuni za soka.
Akilimali
amesema Yanga ni timu bora kwa sasa katika ukanda wa Afrika Mashariki
na Kati kila mmoja anajua hilo, tuna wachezaji wazuri wenye kiwango cha
hali ya juu ambao wamepikwa wakapikika wakaiva matunda ya mafunzo yao
ndio yaliyotupatia ubingwa kabla ya ligi kumalizika.
Aidha
aliongeza kuwa "Tunaahidi kwamba tutamfunga Simba SC siku ya mei 18
kutokana na umoja wetu, mshikamano na uongozi bora chini ya mwenyekiti
Yusuf Manji na makamu wake Clement Sanga ambao mpaka sasa wameifnaya
timu ya Yanga kuwa ya kuogopewa ukanda wote huuu".
Naye
Mzee Hashim Mwika aliongeza kuwa waanahidi ushindi katika mchezo huo,
idadi ya mabao haijalishi lakini kikubwa tunasema lazima tumfunge Simba
mei 18 kikubwa tunaomba mwamuzi achezeshe kwa kufuata kanuni 17, na kama
wakifanya hivyo basi Simba Sc wajiandae kupokea mvua ya mawe siku hiyo.
"Mwaka
jana walitufunga kwa sababu hatukuwa pamoja, hatukua na maelewano
lakini hivi sasa Yanga ni moja kuanzia viongozi, wachezaji, makocha na
wanachama hivyo tunamini kwa kuwa pamoja na timu yetu bora lazima simba
achezee kichapo "alisema mzee Mwika.
chanzo:www.youngafricans.co.tz
إرسال تعليق