Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Kundi la
Vijana Mkoa wa Arusha, Catherine Magige aliyeanzisha mjadala.
Na Mwandishe wetu.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Kundi la Vijana Mkoa wa Arusha, Catherine
Magige, ndiye aliyeanzisha mjadala asubuhi katika kipindi cha maswali na
majibu, baada ya kumuuliza Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
kuhusu mpango wa serikali kudhibiti ukahaba.
Magige aliuliza kuhusu fikra za serikali juu ya mpango wa kupeleka
muswada bungeni, kuhusu uundwaji wa sheria ya kudhibiti ukahaba nchini.
Swali hilo la Magige, lilikwenda sambamba na maelezo kuwa biashara ya
ukahaba inavyoshamiri, inazidi kusababisha mmomonyoko mkubwa wa maadili.
Alisema, biashara hiyo vilevile ni kichocheo cha kushamiri kwa maambukizi
ya Virusi Vya Ukimwi, kuongezeka kwa watoto wa mitaani na kukua kwa uha
lifu kwa
sababu kuna uporaji hufanyika kwa kuwatumia hao wanaojiuza.
Akijibu swali hilo kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na
Watoto, Sophia Simba, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki alisema
serikali inajitahidi kuimaliza biashara ya ukahaba nchini.
SPIKA wa Bunge, Anne Makinda.
Aliongeza kuwa serikali inatumia
taasisi mbalimbali za kijamii kuielimisha jamii kuhusu athari za ukahaba.
Magige, aliuliza maswali mawili ya
nyongeza, moja akitaka kutungwa kwa adhabu kali, maana zile zitolewazo sasa
zimeonekana ni dhaifu, pili akataka takwimu ya kesi za ukahaba ambazo
zimesharipotiwa mpaka sasa.
Akijibu maswali hayo, Kairuki alisema
kuwa umuhimu wa kutoa adhabu kali ni mkubwa lakini akasema tatizo ni jamii,
kwani imekuwa ikiyajua madanguro ya makahaba lakini watu hawatoi ushirikiano.
Kuhusu takwimu, Kairuki alisema kuwa
mwaka jana, ndani ya Jiji la Dar es Salaam, kesi 22 ziliripotiwa Mahakama ya
Jiji na watuhumiwa 123 walihukumiwa.
Wakati huohuo, baadhi ya machangu
wameliambia Amani kuwa watakuwa wakitembea na tindikali kama nyenzo ya
kujilinda wanapokuwa katika shughuli zao.
إرسال تعليق