KAMPUNI YA COCA COLA MBEYA YAKARABATI KITUO CHA POLISI IYUNGA JIJINI MBEYA







Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya  Barakaeli Masaki wakipeana mkono na Mkurugenzi uzalishaji wa kampuni ya cocacola  Lovis Cotyee mara baada ya kukabidhiwa kituo hicho






Kaimu kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ndugu Barakaeli Masaki ameishukuru kampuni hiyo kwa msaada wao katika kuimlaisha ulinzi na usalama katika jiji la mbeya.

Mkuu wa kituo cha Polisi Iyunga Laison Kasimbilu
Akizungumza katika makabidhiano ya kituo cha polisi Iyunga jijini Mbeya  Ndugu Haji Ally Promosheni Meneja kutoka  Kampuni vinywaji baridi ya Coca cola ambayo imefadhili ukarabati wa kituo hicho kilicho gharimu kiasi cha shilingi milioni 10 amesema wao kama kampuni wametoa msaada huo kwa lengo kurudisha kile walicho kipata ndani ya jamii.









Baadhi ya wakazi wa Iyunga walishuhudia tukio hilo

Wito umetolewa kwa wadau mbalimbali na wananchi  mkoani mbeya kuhakikisha wanatoa michango yao katika kuhakikisha jeshi la polisi linaendelea kuimalisha ulinzi na usalama kwa jamii.
  
Michango hiyo ni pamoja na kujenga vituo vya Polisi na ukarabati ambao utaweza kutoa fursa kwajeshi hilo kufanya kazi kwa bidii katikakuhakikisha jamii inaendelea kuishi maeneo salama na tulivu.
  
Akizungumza katika makabidhiano ya kituo cha polisi Iyunga jijini Mbeya  Ndugu Haji Ally Promosheni Meneja kutoka  Kampuni vinywaji baridi ya Coca cola ambayo imefadhili ukarabati wa kituo hicho kilicho gharimu kiasi cha shilingi milioni 10 amesema wao kama kampuni wametoa msaada huo kwa lengo kurudisha kile walicho kipata ndani ya jamii.
Amesema yapo maeneo mbalaimbali ambayo wameweza kusaidia jamii hasa katika sekta ya elimu .afya  pamoja na maeneo mengine hivyo kitendo cha wao kusaidia jeshi hilo la polisi ni kama muendelezo wa matukio yanayo fanywa na kampuni hiyo .
 Meneja huyo ameyataka mashirika mbalimbali mkoani humu kuhakikisha wanasaidia maeneo yanayo hitaji misaada kama ambavyo wao wameweza kuonyesha mfano kwa kukarabati kituo hicho cha Iyunga ambacho awali kilikuwa katika hali mbaya.
  
Amebainisha kuwa msaada huo haujaishi kwa jeshi la polisi pekee kwani bado kuna maombi mbalimbali ndani ya jamii ambayo yanahitahi kupatiwa misaada kutoka katika kampuni hiyo hivyo ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano wao katika kuijenga  jamii ya mkoa wa mbeya.
Kwa uapande wake kaimu kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ndugu Barakaeli Masaki ameishukuru kampuni hiyo kwa msaada wao katika kuimlaisha ulinzi na usalama katika jiji la mbeya.
Amesema mchangho ulio tolewa na Kampuni hiyo ni mkubwa kwani umeweza kuboresha mazingira bora ya kituo hicho na kulifanya jeshi hilo kufanya kazi zake  kwa usanifu.

Pia amezitaka taasisi mbalimbali pamoja na mashirika mengine kuendelea kutoa michango yao kwa jeshi la polisi mkoani humo ikiwa ni pamoja na kuimalisha vituo vingine vya polisi ambavyo hali yake hairidhishi.

Picha na Mbeya yetu

Post a Comment

Previous Post Next Post