Shindano
la kumtafuta Miss Tabata 2013 linafanyika leo katika ukumbi wa Dar West
Park Tabata. Warembo 20 watachuana kutaka kumrithi Noela Michael ambaye
anashikilia taji hilo kwa sasa. Noela pia ndiye anashikiria taji la
Miss Ilala.
Mbali
ya kuwakilisha Miss Tabata kwenye shindano la Miss Ilala baadaye mwaka
huu, mshindi huyo pia atazawadiwa Sh.600,000 pamoja na king’amuzi kutoka
Multichoice ambacho kimelipiwa tayari kwa miezi mitatu kikiwa na
thamani ya Sh.400,000.
Mshindi pili atapata Sh. 300,000, wa nne Sh.200,000 na wa tano atazawadiwa Sh.150,000. Warembo
wengine watakaofanikiwa kuingia 10 bora, watazawadiwa Sh.100,000 kila
mmoja wakati waliosalia watapata kifuta jasho cha Sh.50,000 kila mmoja.
Warembo
wanaoshiriki kinyang’anyiro hicho mwaka huu ni Madgalena Bhoke (21),
Kabula Juma Kibogoti (20), Upendo Dickson Lema (22), Hidaya David Mwenda
(22), Aneth Ndumbaro (19), Dorice Mollel (22), Eunice Nkoha (19),
Kazunde Musa Kitereja (19), Rehema Kihinja (20), Pasilida Mandali
(21), Brath Chambia (23), Joaniter Kabunga (21), Recho Mushi
(20),Caroline Sadiki (20) na Suzan Daniel (18).
Wadhamini
wa shindano hilo ni Dodoma Wine, Redd’s Original, Nipashe, Vayle
Springs, Multichoice, Fredito Entertainment, Integrated Communications
Limited, CXC Africa, Brake Point na Saluti5.
Miss Tabata 2013 imeandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts.
Post a Comment