REDD'S MISS LINDI 2013 KUPATIKA USIKU WA LEO

Washiriki wa Redd’s Miss Lindi 2013 katika picha ya pamoja ndani ya ufukwe wa Lindi Beach Resort
Redd’s Miss Lindi 2013 atajulikana Usiku wa leo 31 may,2013 ndani ya ukumbi wa Lindi Beach Resort. 

Jumla ya Warembo Kumi watachuana Vikali kugombania taji hilo. wanyange hao wako kambini Hotelini hapo kwa mazoezi makali huku wakiongozwa na Redd’s Miss Lindi 2012.

Mratibu wa Mashindano hayo Ndugu Justine alisema Mwaka huu wamejiandaa vizuri na warembo wako katika hali nzuri ya kiafya kambini hapo na Pia anataraji show itakuwa ya Kihistoria kwa jinsi maandalizi yalivyo andaliwa, hivyo amewataka wadau kujitokeza kwa wingi.
Viingilio vimetajwa kuwa viti vya kawaida siku hiyo vitakuwa Tsh 10,000/= na VIP itakuwa 15,000/= na tiketi zitaanza kuuzwa siku hiyo hiyo ya tarehe 31/05/2013 majira ya asubuhi Hivyo wahi tiketi yako mapema ili ushuhudie show ya kihistoria katika mambo ya urembo katika mji wa Lindi.

Post a Comment

Previous Post Next Post