Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kushoto) katika mazungumzo na Balozi
wa Canada nchini Tanzania Mhe Alexandre Leveque aliyemtembelea ofisini
kwake Ikulu jijini Dar es salaam leo asubuhi. Balozi Leveque aliongozana
na Mkurugenzi Mwandamizi na Mkuu wa Ushirikiano wa Canadian
International Development Agency (CIDA), Bi Patricia McCullagh. Wa pili
kushoto ni Balozi Dorah Msechu, Mkurugenzi
katika Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
anayeshughulikia kurugenzi ya Nchi za Ulaya na Amerika, akifuatiwa na ofisa dawati Bi Upendo Mwasha. Picha na Ikulu
إرسال تعليق