Meneja
wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe (kushoto)
akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. Mil. 25 kwa Katibu Mkuu
wa Yanga,Laurance Mwalusako kama zawadi ya ubingwa wa Ligi
Kuu.Wanaoshuhudia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga,Mussa
Katabaro (wa pili kutoka kulia) ,Mkurugenzi wa Fedha Yanga,Denis Oundo
pamoja na Geoffrey Makau (wa pili kutoka kushoto).
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL)
kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro Lager imewazadiwa sh milioni 25
mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, klabu ya soka Yanga.
Akizungumza katika hafla ya
kukabidhi hundi hiyo, Meneja wa kinywaji cha Kilimanjaro, George Kavishe
alisema kwamba zawadi hiyo ni sehemu ya ahadi ya udhamini wao kwa timu
itakayoshinda ama kushika nafasi za juu.
“Kama
wadhamini wa klabu kongwe za yanga na Simba tuliahidi kutoa mil 25 timu
itakayotwaa ubingwa wa Ligi kuu n ash mil 15 kwa timu itakayoshika nafasi ya
pili, hivyo kutokana na Yanga kutwaa ubingwa ndio tunaikabidhi fedha hizi,”alisema.
Kavishe aliongeza zawadi hiyo
ni sehemu sh bilioni 1.5 ya udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager kwa Yanga na
imetolewa kwa lengo la kuhamasisha klabu kujitahidi kwa ushindi zaidi na
kusaidia klabu katika maandalizi yake kwa ajili ya mashindano ya kimataifa.
“na tulifanya hivi makusudi
ili kuleta ushindani kwa timu hizi za
Simba na Yanga ili ziweze kufanya vema
kwenye ligi hiyo ambayo imekuwa na ushindani mkubwa.
“Yanga imekuwa ikicheza mpira
mzuri kipindi chote cha msimu wa ligi kuu na hivyo kuibuka washindi.Napenda
kuwapongeza wachezaji, kocha na uongozi mzima wa Yanga kwa matokeo mazuri ya
kushinda ligi kuu kwa mara ya 24 sasa,”alisema.
Akipokea hundi hiyo,Katibu
Mkuu wa Yanga,Lawrance Mwalusako, pamoja
na kushukuru alisema Yanga ni timu nzuri na yenye nguvu kutokana na uongozi
imara pamoja na udhamini wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
“mafanikio yetu ya uwanjani
ni ikielelezo cha mafanikio pia ya bia ya Kilimanjaro Premium Lager kwa ujumla
ambayo imekuwa ikitusaidia sana.Bia hii imetoa mchango mkubwa sana katika kuipa timu msukumo uliopelekea
mafanikio haya,”alisema.
Mwalusako aliongeza kuwa,
Yanga kwa sasa ina nafasi ya kuonekana kwenye jukwaa la kimataifa la soka
kutokana na udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager hivyo itaendelea kukua na
kufanikiwa.
Kwa ubingwa huko Yanga
itaiwakilisha Tanzania kwenye ligi ya mabingwa Afrika mwakani, pamoja na
michuano ya klabu bingwa ya Afrika Mashariki na Kati maarufu kama Kombe la
Kagame inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia juni 18 hadi Julai 2 huko
Sudan Kusini ambapo Yanga ni mabingwa watetezi.
Mbali na zawadi hiyo ya TBL, Yanga inatarajiwa kupata kitita cha sh milioni 70 kutoka kwa wadhamini wakuu wa Ligi hiyo, kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.
إرسال تعليق