Wafuasi wa Chadema Iringa
wakiwa wamembeba juu juu mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji
Peter Msigwa baada ya kuachiwa kwa dhamana leo hadi kesi hiyo
itakapotajwa tena Juni 3 mwaka huu huku wafuasi wake 26 kati ya 74
wakosa sifa ya dhamana
Mbunge Msigwa akishuka katika gari ya polisi huku akiwa chini ya
ulinzi mkali wa FFU leo alipofikishwa mahakamani kabla ya
kudhaminiwa
Mheshimiwa mbunge Msigwa akishuka katika gari ya polisi chini ya ulinzi mkali wa polisi
Mkuu wa FFU Iringa Said Abdalah Mnunka (katikati) akiwa na maofisa wenzake wa polisi
Katibu wa Chadema wilaya ya Iringa mjini Bi Suzana Mgonakulia akitoa nje ya mahakama hiyo
|
mbunge Msigwa akiwa amebebwa juu juu na wafuasi wa Chadema jioni hii
SAKATA la vurugu za machinga na polisi
mjini Iringa limechukua sura mpya baada ya jeshi la polisi mkoa wa
Iringa kumfikisha mahakamani mbunge wa jimbo la Iringa mjini
mchungaji Peter Msigwa pamoja na watuhumiwa wengine zaidi ya 70
Huku mahakama hiyo ikitoa masharti
nafuu ya dhamana kwa watuhumiwa hao na kuwaonya kutofanya kosa kwa
kipindi chote cha kesi hiyo inapoendelea kusikilizwa .
Watuhumiwa hao walifikishwa katika
mahakama ya hakimu mkazi wa wilaya ya Iringa Mheshimiwa Godfrey Isaya
leo majira ya saa 8 mchana huku wakiwa chini ya ulinzi mkali wa
askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) waliokuwa na msafara wa
magari zaidi ya matatu likiwemo gari ya maji ya kuwasha .
Mbali ya mbunge Msigwa kupanda gari
ndogo ya wazi ya polisi pamoja na watuhumiwa wawili wanawake
waliokamatwa katika vurugu hizo bado watuhumiwa wengine 74
walitumia usafiri wa karandinga la polisi .
Mbele ya mahakama hiyo wakili wa
serikali Adolph Maganda alisema kuwa watuhumiwa hao kwa pamoja
wanatuhumiwa kwa kosa kwa makosa matatu likiwemo la kufanya
kushiriki mkutano na kufanya vurugu ,uchechezi na kuharibu mali
kinyume na sheria
Huku mbunge akisomewa mashitaka mawili likiwemo kushawishi na kufanya mkutano bila kibali .
Watuhumiwa wote wamekana mashitaka
dhidi yao huku wakili wa serikali akidai kuwa hana pingamizi na
dhamana kwa watuhumiwa hao wote hata hivyo wote wamekana
mashitaka yote yaliyotolewa dhidi yao .
Hata hivyo makimu anayesikiliza kesi
hiyo alisema kuwa dhamana kwa washitakiwa wote ipo wazi kwa kila
mmoja kuwa mdhamini mmoja anayeaminika pamoja na kusaini hati ya
dhamana ya Tsh milioni moja .
Hadi majira ya saa 10 jioni mahakama
hiyo ilikuwa ikiendelea na mchakato wa kupitia barua za dhamana
kwa wadhamini huku mbunge akiwa wa kwanza kudhaminiwa ,mbali ya
mbunge watuhumiwa kati ya 74 waliokuwa bado kupata wadhamnini ni
watuhumiwa sita pekee.
Katibu wa chama cha Demokrasia na
maendeleo (Chadema) wilaya ya Iringa mjini Suzana Mgonakulima alisema
kuwa mchakato wa kuwadhamini watuhumiwa wote waliosalia
unaendelea kufanyika na kuwa wana uhakika wa watuhumiwa wote
kudhaminiwa .
Hadi majira haya ya saa 10 .40
mbunge msigwa na wengine wameachiwa huku watuhumiwa 26 kati ya 74
wamekosa dhamana hadi kesi hiyo itakapotajwa tena tarehe 3 /6/2012
Wakati huo huo wananachi waliofika
mahakamani hapo kushuhudia mbunge wao akifikishwa mahakamani
wamempongeza mkuu wa kikosi cha kutuliza ghasia mkoa wa Iringa (FFU)
Said Abdulah Mnunka kwa kusimamia amani na utulivu katika eneo hilo la
mahakama na jinsi ambavyo alivyoweza kupambana na machinga pasipo
kumwaga damu kwa siku ya jana wakati wa vurugu hizo
|
إرسال تعليق