Ndoa ya Jimmy Mafufu yajibu! Apata mtoto wa kiume, ampa jina la mchezaji mpira maarufu duniani.

Ndoa ya Jimmy Mafufu yajibu! Apata mtoto wa kiume, ampa jina la mchezaji mpira maarufu duniani.



Hatimaye ndoa ya mwigizaji wa bongo movies imezaa matunda mazuri baada ya mke wake Salma kujifungua mtoto wa kiume jana (23/05/2013) majira ya saa tatu (3) usiku katika hospitali ya temeke jijini Dar es salaam.
Akiongea na mwandishi wa habari hii Jimmy alisema kuwa mama wa mtoto na mtoto wanaendelea vizuri na anamshukuru sana Mungu kwa Baraka hiyo katika ndoa yake.
Alipoulizwa zaidi kuhusu mtoto, Jimmy alisema kuwa, amepanga kumpa mtoto wake huyo jina la Ronaldo kwani yeye ni mpenzi mkubwa sana wa mpira wa miguu.
Jina hili ni maarufu sana kwa wapenzi wa mpira wa miguu kwani nyota kadhaa wa mpira ulimwenguni wenye jina kama hili wamepata nafasi ya kuwika na kuwa wachezaji bora wa dunia kama vile mbrazili Ronaldo de lima, na Christiano Ronaldo wa Ureno.
(Kutokana na sababu za kiafya hatukuweza kumpiga picha mtoto huyo aliyezaliwa jana)
Hongera sana Jimmy Mafufu.

Post a Comment

أحدث أقدم