RAIS
WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE
KUZINDUA MIRADI YA UJENZI WA BARABARA YA DODOMA – IRINGA YENYE UREFU WA KM 260
(SEHEMU ZA DODOMA - FUFU ESCARPMENT, FUFU ESCARPMENT - MIGORI NA MIGORI -
IRINGA) KWA KIWANGO CHA LA
Wizara ya Ujenzi inapenda kutoa taarifa kwa Umma kwamba, tarehe 22 Mei, 2013 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete atakuwa mgeni Rasmi katika sherehe za uzinduzi wa miradi ya ujenzi wa barabara kama ifuatavyo:-
1) Tarehe
22 Mei, 2013 Asubuhi kuweka jiwe la msingi sehemu ya Dodoma – Fufu Escarpment
(km 93.8) katika eneo la Dodoma Mjini.
2) Tarehe
22 Mei, 2013 Mchana kuweka jiwe la msingi sehemu ya Fufu Escarpment
– Migori (km 70.9) na Migori – Iringa (km 95.3) katika Kijiji cha Migori
Wilayani Iringa Vijijini.
Barabara
ya Iringa - Dodoma ni sehemu ya barabara muhimu ijulikanayo kama “Great North
Road” inayoanzia Capetown Afrika ya Kusini hadi Cairo, Misri kupitia Tanzania.
Nchini Tanzania inaunganisha Miji ya Tunduma (mpakani na Zambia), Mbeya,
Iringa, Dodoma, Arusha na Namanga (mpakani na Kenya).
Mradi
huu ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Nne ya kuboresha miundombinu
muhimu ya usafiri wa barabara na unalenga kupanua fursa za kiuchumi na
kibiashara kwa wananchi, na kati ya Tanzania na nchi jirani za Jumuiya ya
Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Kwa
njia hii, barabara itakuza uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Taarifa
hii imetolewa na;
Balozi
Herbert E. Mrango
KATIBU
MKUU
WIZARA
YA UJENZI
إرسال تعليق