Mh Amos Makalla (kushoto ) akiwa na Angetileh Oseah
SHIRIKISHO
la Soka la Kimataifa (Fifa) limeliagiza Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) kuanza upya mchakato wake wa Uchaguzi Mkuu baada ya kubaini mambo
kadhaa lilipokuja kusilikiza malalamiko ya baadhi ya wagombea wa
uchaguzi huo.
Uamuzi
huo wa Fifa ni kama ulikuwa ukitabiriwa na wadau wengi wa michezo
nchini kutokana na madudu yaliyofanywa na Kamati ya Uchaguzi na ile ya
Rufaa ya TFF, kiasi cha baadhi ya wagombea kuamua kupeleka malalamiko
yao Fifa baada ya kutokuwa na chombo chenye mamlaka mengine hapa nchini.
Mvutano
ulizidi kupamba moto baada ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
kuingilia kati.
Kutokana
na hali hiyo, serikali ilipitia upya malalamiko hayo ambayo yalilenga
kubatilisha uamuzi wa TFF kuendesha uchaguzi huo kwa kutumia marekebisho
ya katiba yaliyofanyika mwaka 2012 kwa njia ya waraka uliosambazwa
kwenye mikoa yote wanachama wa TFF.
Tofauti
na katiba inavyosema kwamba, ili marekebisho ya katiba yafanyike, ni
lazima mkutano mkuu ukae, TFF ilipitisha marekebisho hayo bila ya
mkutano mkuu kukaa kwa maelezo kwamba hawana fedha za kuendesha mkutano
huo.
Serikali
iliagiza kutotumiwa kwa katika hiyo ya mwaka 2012, hapo ndipo
palipoibuka malumbano kati ya Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Mh. Amos Makalla na Katibu Mkuu wa TFF, Angetile
Osiah.
Angetile
ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari alikuwa akijibizana wazi wazi
na Mh. Makalla huku akijua kwamba kinachofanywa na waziri huyo ni
maagizo ya mabosi wake ambao ni waziri husika, Dr Fenella Mukangara na
serikali kwa ujumla.
Hatukupenda
majibizano hayo kwa kuzingatia vitu viwili, kwanza, TFF ipo chini ya
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, hivyo kuendeleza
malumbano kwa Angetile na Mh. Makalla hakukuwa na manufaa ya kukuza soka
la Tanzania.
Ni
malumbano ambayo Angetile hakupaswa kuyapa nafasi kwa kuwa serikali
ndiyo inayoratibu kila kitu kinachohusu michezo nchini na hata uamuzi wa
kuipiga ‘stop’ katiba ya 2012 lilikuwa jambo sahihi ambalo hata Fifa
waliliona baadaye.
ANGETILEH ALIKUWA AKIBISHANA NA SERIKALI
Angetileh
alipokuwa akilumbana na kujibizana na Mh. Makalla tunadhani alisahahu
kwamba Makalla anafanya kazi chini ya serikali ya Rais Jakaya Kikwete,
hivyo kupingana na kujibizana na mtu kama huyo ni sawa na kujibizana na
serikali iliyo chini ya Mh. Kikwete.
Kama chombo cha habari, www.shaffihdauda.com
tunadhani Angetile atakuwa amejifunza kutokana na jambo hili na kwa
kuzingatia taaluma yake anapaswa kuviomba radhi vyombo vya habari, kwani
wadau wa soka walikuwa wakimtazama Angetileh kwa macho mawili kwanza
akiwa kama katibu mkuu wa TFF pili akiwa kama mwandishi ‘ Senior ‘ wa
habari za michezo.
Kitendo
kile kilitoa picha mbaya kwa waandishi wa habari karibu wote, hasa
wanaondika habari za michezo. Tunasisitiza hii haikuwa picha nzuri kwa
taaluma.
Hakukuwa
na haja ya Angetile kubishana na Mh. Makalla kama angekuwa anafahamu
anayebishana naye ni naibu waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo, ambayo kimsingi hata yeye Angetile, Mh. Makalla ni kama
bosi wake.
Hatujuhi
ilipopatikana nguvu ya Angetile kubishana na Mh. Makalla huku
akimdharau naibu waziri huyo kwa kusema hata akienda wizarani
atazungumza na waziri husika na siyo msaidizi wake.
Hoja
ya kwamba, Mh. Makalla alikuwa akiegemea upande mmoja haikuwa na
mashiko kwani uamuzi wa kutotumia katiba ya mwaka 2012, ulipata pia
baraka za Mh. Dr Mukangara na Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
MSIMAMO WETU
Tunaamini
kwamba, Angetile ni binadamu kama walivyo binadamu wengine hivyo
atakuwa amebaini kosa alilofanya katika jambo hili hivyo kutorudia tena
endapo hali kama hii itajitokeza hapo baadaye (kama atabaki madarakani).
Tutaendelea
kusimamia haki katika michezo bila kupindisha ukweli na kamwe hatuwezi
kuzifanyia kazi kelele za watu wengine ambao kwa namna moja au nyingine
hawana nia nzuri na soka la Tanzania.
إرسال تعليق