Uhalali wa Taifa la Tanzania katika karne 21


Na Amin Ally Washington Seattle

Jee tunahitajia kujitawala kwa misingi ya migawanyiko ya kidini baina ya Watanzania...?

Taifa la Tanzania linaweza kumkumbuka za baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa nasaha zake kuhusu masuala ya Udini hakika mengi ambayo ameongea katika uhai wake sasa yanaanza kujitokeza kwa Watanzania ndani na nje kutokana kuingizwa kwa vitendo vya kuvunja amani na kuwepo vyama ambavyo havina Dira sahihi kwa wananchi wa Tanzania.

Katika karne hii ya 21 kuna watu wachache ambao wanaona Dini zao ni bora zaidi kuliko nyengine, napenda kutoa nasaha zangu kama raia Mwema Tanzania ikingia katika mfumo wa kidini katika kuongoza taifa letu tunaweza kushindwa kujitawala wenyewe ndani ya Taifa letu na kugawa wananchi kutokana tofauti za kidini na hilo ndio ambalo limetokea huko Nigeria , Bosnia , Lebanon , Pakistan , na mataifa mengine duniani.

Watanzania tunakaribisha matokea kama haya katika jamii na mikoa yetu bila shaka damu ikitokea kumwagika hatutoweza kusahaulika katika jamii zote za kidini na kubakia katika imani za watu wenye taifa moja na mfumo wa ibada tofauti.


Tunawaomba vyama vyenye milango ya kidini katika taifa la Tanzania kuachana na hoja za kidini katika siasa zao hutoweza kutawala kutokana na sera ya kidini katika taifa la Tanzania bali unaweza kuongoza wananchi wa taifa la Tanzania kwa sera za kikatiba na mamlaka ya kiuchumi na kuondoa umaskini.

Vile vile tunawaomba waTanzania wote wenye dini tofauti kutizama nchi yetu Tanzania inataka nini katika karne 21 na kuendelea kugawa taifa letu kidini au kuchukua fursa mpya ya mabadiliko ya kiuchumi yanayoingia katika bara la Afrika.

Jee waTanzania tumejifunza kwa wakenya tangu kupata uhuru hadi sasa katika masuala la ukabila ? 
Jee tunaweza kutatua matatizo ya kidini wenyewe au kupokea shindikizo la mataifa makubwa ?

Jukumu la kudumisha Amani linakuja kwa dini za waTanzania au Taifa lenye kuunda dini tofauti katika maisha ya Watanzania ?

(Tunawaomba kutoa hoja zenu zinye misingi ya kuleta AMANI  kwa waTanzania ili kutupa changamoto  katika hoja hii)

Post a Comment

Previous Post Next Post