Na Amin Ally Washington Seattle
Jee tunahitajia kujitawala kwa misingi ya migawanyiko ya kidini baina ya Watanzania...?
Taifa la Tanzania linaweza kumkumbuka za baba wa taifa Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere kwa nasaha zake kuhusu masuala ya Udini hakika mengi
ambayo ameongea katika uhai wake sasa yanaanza kujitokeza kwa Watanzania
ndani na nje kutokana kuingizwa kwa vitendo vya kuvunja amani na kuwepo
vyama ambavyo havina Dira sahihi kwa wananchi wa Tanzania.
Katika karne hii ya 21 kuna watu wachache ambao wanaona Dini zao ni bora
zaidi kuliko nyengine, napenda kutoa nasaha zangu kama raia Mwema
Tanzania ikingia katika mfumo wa kidini katika kuongoza taifa letu
tunaweza kushindwa kujitawala wenyewe ndani ya Taifa letu na kugawa
wananchi kutokana tofauti za kidini na hilo ndio ambalo limetokea huko
Nigeria , Bosnia , Lebanon , Pakistan , na mataifa mengine duniani.
Watanzania tunakaribisha matokea kama haya katika jamii na mikoa yetu
bila shaka damu ikitokea kumwagika hatutoweza kusahaulika katika jamii
zote za kidini na kubakia katika imani za watu wenye taifa moja na mfumo
wa ibada tofauti.
Tunawaomba vyama vyenye milango ya kidini katika taifa la Tanzania
kuachana na hoja za kidini katika siasa zao hutoweza kutawala kutokana
na sera ya kidini katika taifa la Tanzania bali unaweza kuongoza
wananchi wa taifa la Tanzania kwa sera za kikatiba na mamlaka ya
kiuchumi na kuondoa umaskini.
Vile vile tunawaomba waTanzania wote wenye dini tofauti kutizama nchi
yetu Tanzania inataka nini katika karne 21 na kuendelea kugawa taifa
letu kidini au kuchukua fursa mpya ya mabadiliko ya kiuchumi yanayoingia
katika bara la Afrika.
Jee waTanzania tumejifunza kwa wakenya tangu kupata uhuru hadi sasa katika masuala la ukabila ?
Jee tunaweza kutatua matatizo ya kidini wenyewe au kupokea shindikizo la mataifa makubwa ?
Jukumu la kudumisha Amani linakuja kwa dini za waTanzania au Taifa lenye kuunda dini tofauti katika maisha ya Watanzania ?
(Tunawaomba kutoa hoja zenu zinye misingi ya kuleta AMANI kwa waTanzania ili kutupa changamoto katika hoja hii)
إرسال تعليق