
Vikosi vya Kulinda Amani vya Umoja wa
Afrika na Umoja wa Mataifa UNAMID huko Darfur Sudan vimeyataka makundi
ya waasi kusitisha machafuko na vitendo vya utumiaji mabavu.
Taarifa ya UNAMID imezitaka pande zote zinazozona katika jimbo la Darfur
hususan makundi yanayobeba silaha na ambayo hayajajiunga na hati ya
makubaliano ya amani kusitisha vitendo vya hujuma na kuheshimu sheria za
kimataifa.
Taarifa ya Vikosi vya Kulinda Amani vya Umoja wa Afrika na Umoja wa
Mataifa UNAMID huko Darfur Sudan imesisitiza juu ya himaya ya Umoja wa
Afrika, Umoja wa Mataifa na jamii ya kimataifa kwa hati ya makubaliano
ya amani ya Darfur iliyotiwa saini katika mji mkuu wa Qatar, Doha.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, mwanzoni mwa mwezi huu wa Mei zaidi ya
watu 130 waliuawa baada ya kutokea mapigano ya kikabila katika jimbo
la Darfur magharibi mwa Sudan.
إرسال تعليق