STAA wa filamu za Kibongo, Irene Uwoya haachi vituko, safari hii
ameibuka na kujisafisha kupitia Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza
akidai kuwa yeye na tasnia nzima ya sinema za Kibongo hawana tabia za
hovyo bali Magazeti Pendwa ndiyo yanasababisha waonekana hivyo.
irene Uwoya.Pamoja na skendo nyingine, Uwoya hivi karibuni alinaswa
kwenye mtego baada ya kuingia kwenye kumi na nane za kamera za
mapaparazi wa Global Publishers akiwa na kinda la muziki wa Bongo Fleva
Nasib Abdul ‘Diamond’ wakiingia katika hoteli moja jijini Dar usiku
mnene na kutoka mchana wa siku iliyofuata.
Akizungumza hivi karibuni kupitia runinga moja jijini Dar es Salaam,
Uwoya alijitetea kwamba sanaa ya filamu za Kibongo ni safi na kwamba
magazeti ndiyo yanayowaharibia sifa.

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza.“Mfano mimi, kama ningekuwa mchafu
ningeitwa na rais wa Burundi kwenda ikulu? Ameniona mimi ni msafi ndiyo
maana aliniita mwaka 2011 kupitia sanaa yangu. Tungekuwa wachafu
tusingekubalika hadi na viongozi wakubwa wa nchi, tatizo ni magazeti,”
alisema Uwoya akijibu swali la mtangazaji wa kipindi hicho, aliyetaka
kujua kuhusu madai ya wasanii kuwa na tabia chafu.
Uwoya ni kama alikuwa akikwepa hoja ya msingi na kuyatupia lawama
Magazeti Pendwa kwa kuegemea mgongo wa Rais Nkurunzinza, kwa sababu
rekodi za skendo zake zipo na yeye mwenyewe anazijua – Mhariri.

إرسال تعليق