Baadhi ya walimbwende wa wilaya ya Mbeya Vijijini wakiwa katika pozi, wana urefu, shepu na haiba za kuvutia hakika kinyang'anyiro kitakuwa kigumu.....
Wadau mnaona mambo haya?!!!
Katikati ni Sarah Kalinga ambaye ni Mkurugenzi na mratibu wa Miss Redds 2013 Mbeya Vijijini ambaye pia anaongoza kampuni ya Mama Neema Decoration..
WALIMBWENDE 12 wanatarajia kuwania taji la Miss Redds 2013 katika wilaya ya Mbeya Vijiji mkaoni hapa, linalotarajia kufanyika katika ukumbi wa Royal Tughimbe Mei 24, mwaka huu mjini Mbalizi wilayani humo.
Mkurugenzi na mtaribu wa shindano hilo Sarah Kalinga kupitia kampuni ya Mama Neema Decoration Interprises, aliliambia Tanzania Daima jana kuwa maandalizi yanaendelea na tayari warembo wameingia kambini.
Alisema warembo wote waliojitokeza mwaka huu wana sifa zinazolingana na wanashindwa kuwachuja tofauti na miaka mingine iliyopita ambapo walikuwa wanakuwa na warembo tisa katika kambi yao.
Alivitaja vigezo vya warembo hao kuwa ni elimu, mwonekano, kimo, nidhamu, kujiamini na kigezo kingine ni kipaji.
‘’Sifa ambazo zinaweza kumuondoa mrembo kambini na kumfuta katika ushiriki wa mashindano ni ulevi, matumizi ya simu, kutembelewa na boyfried, wizi, uchafu na kauli mbaya kwa wenzao na hata wakufunzi wao’’ alisema Sarah.
Alisema mbali na uhitaji wa wadhamini katika shindano hilo kuanzia sasa ambapo warembo wapo kambini, baadhi ya wadhamini wamejitokeza wakiwemo TBL, SBC, Mbaspo,Access Computer, Tuhimbe Hotel, River side Mbalizi, Grace College, Mjasiliamali Sanga,Overcado Saloon, Royal Berbershop, mtandao wa na Royal Berbershop
Alipoulizwa changamoto zaidi alisema kuwa ni kukatwa majina ya warembo kutoka wilayani wanapokuwa katika mashindano ya mkoa kwenda kanda hali ambayo alisema ni vema ikatazamwa na waandaaji wa ngazi hizo.



Post a Comment