WAKATI
Simba na Yanga SC zinakwenda mbio kusajili wachezaji wapya, washindi wa
pili mara mbili mfululizo katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara,
Azam FC wao wamesema hawasajili hata mchezaji mmoja, zaidi watapandisha
wachezaji kutoka katika akademi yao.
Katibu
wa Azam FC, Nassor Idrisa ameiambia BIN ZUIBEIRY leo asubuhi kwamba,
kocha Muingereza Stewart Hall amesema kwa sasa hakuna umuhimu wa
kusajili, zaidi ya kuiangalia timu kwanza katika mzunguko wa kwanza wa
Ligi Kuu, unaotarajiwa kuanza Agosti.
Nassor
amesema kwamba kocha amewaambia iwapo atagundua kuna mapungufu katika
timu katika kipindi cha kuanzia Agosti, ndipo atasajili Novemba katika
dirisha dogo.
“Unajua
mwakani ndio tutakuwa na haya mashindano ya Afrika (Kombe la
Shirikisho). Na pia ndio mbio za ubingwa wa Ligi Kuu (Bara) zinapamba
moto. Kwa hiyo mwalimu ameomba hicho ndicho kipindi kizuri
kusajili,”alisema.
Hata
hivyo, Nassor alisema kwamba kocha amependekeza wachezaji kadhaa
wasajiliwe kutoka katika akademi ya klabu hiyo, wakiwemo Mudathir Yahya
ambaye yupo na timu ya taifa Ethiopia, kipa Hamad Kadebi na Dissmas
ambaye kwa sasa yuko kwenye majaribio Ujerumani.
“Tuna
vijana wengi wazuri katika akademi yetu, mwalimu anawapa nafasi sasa.
Anaamini timu yake ipo vizuri na hana haja ya kuhangaika kutafuta
wachezaji wapya,”alisema Nassor.
Mudathir
pia alikuwa kwenye majaribio nchini Ujerumani, akarudishwa nchini
kujiunga na timu ya taifa, Taifa Stars kujiandaa kwa mchezo wa kuwania
tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Ethiopia.
SOURCE; BIN ZUBEIRY
إرسال تعليق