WATEJA WA NDEGE ZA FASTJET SASA KUKATA TIKETI ZAO KWA NJIA YA TIGO PESA

Meneja wa chapa ya tigo , Bw William Mpinga ( Kushoto) akiwa na Meneja Mkuu wa fastjet Tanzania , Tim Lee Foster (kulia) wakati wa uzunduzi wa huduma mpya ambayo itawawezesha wateja wa Tigo kununua tiketi ya ndege za fastjet kupitia huduma ya Tigo.
William Mpinga na Tim Lee Foster(kati ya picha) wakipiga picha ya pamoja na wakilishi kutoka kampuni ya Tigo na fastjet Tanzania mwishoni wa unzinduzi wa huduma mpya inayo wawezesha wateja wa Tigo kununua tiketi ya ndege za fastjet kupitia huduma ya Tigo .

*******    ******
Kampuni ya simu ya za mkononi Tigo Tanzania, leo imeingia ubia na shirika ya ndege Fast-jet  na kutangaza ushirikiano wao mpya  ambao sasa mteja anaweza kununua tiketi yake ya ndege za Fast Jet kupitia huduma ya Tigo.
 

Meneja waChapa ya Tigo Tanzania Bw. William Mpinga alisema “ kwenye ushirikiano huu Tigo imekuwa kwa kiasi kikubwa kwa kipindi hiki na imeona uwiano na Fastjet kama fursa kubwa ya kuongeza huduma kwa wateja wetu ambao wanafikia zaidi ya milioni sita”  . 


Kuwa kampuni ya simu  inayoongoza kwa ubunifu Tanzania, dhumuni letu ni  kutoa huduma za simu zenye gharama nafuu ambazo zitaendelea kuboresha maisha ya watanzania.

Ushirikiano huu na Fastjet ni  ushahidi mwingine unaoonyesha jinsi gani tunabuni bidhaa na huduma ambazo zinaleta “urahisi” kwa wateja wetu. Watanzania wameuwa wakiongezeka kwenye huduma za malipo kupitia simu za mikononi nah ii imedhihirishwa na kuongezeka kwa wateja wa Tigo Pesa Tanzania hivyo ushirikiano huu kati ya Tigo Pesa na Fastjet ni muhimu sana kwetu kwasababu ina maanisha kuwa watanzania wengi zaidi wataweza kumudu kusafiri kwa ndege na Tigo Pesa inawapatia urahisi wa kufanya malipo mahali popote walipo.

Akizungumza katika uzinduzi huo , Meneja  Mkuu  wa Fastjet Bwana Tim Lee Foster, “Kampuni ya Fastjet tunaendelea kuwa wabunifu”  Baada ya kupata mafanikio makubwa katika kuingia kwenye  malipo kupitia mitandao ya simu, tumekuwa tukifanya kazi kubwa sana na Tigo kuleta huduma hii muhimu kwa watanzania. 


Zaidi ya asilimia 25% ya wateja wanafanya malipo kupitia mtandao ya simu, na kuzinduliwa kwa huduma hii tunategemea ongezeko la wateja kwa kiasi kikubwa zaidi. Hii imeunganisha na utambolisho wa hivi karibuni wa huduma ya malipo kwa kupitia kadi za benki, hii inaonyesha kuwa wateja wetu sasa wanaweza wakanunua tiketi za ndege za Fastjet kupitia njia nyingi za malipo ambazo zimewekwa kurahisisha malipo hayo.

“Tumetimiza ahadi yetu ya kutoa huduma rahisi kwa wateja wetu kununua tiketi za ndege. Tumewezesha usafiri wa ndege kupatikana kwa urahisi zaidi kwa idadi kubwa ya watanzania pamoja na wageni kutoka nje ya nchi, na tunajivunia kuwa sasa tunalitawala soko la huduma za usafiri wa ndege katika  maeneo ambayo tunasafiri. Tumeonyesha kuwa fastjet inatoa huduma nzuri za kuaminika na kwa bei nafuu”

Bw. William aliongezea akisema kuwa ushirikiano huu kati ya Tigo na fastjet umefanyika kwakuwa mamilioni ya watanzania wanapendelea kutumia  Tigo Pesa kama ilivyoonyeshwa katika ongezeko la watumiaji wa huduma hii. " Ningepengda kuipongeza Fastjet kwa kuona umuhimu wa Tigo Pesa katika maisha ya kila simu ya watanzania na mchango wake mkubwa katika  sekta ya microfinance kama huduma yenye ufanisi mkubwa katika huduma za malipo kupitia mitandano ya  Nataka kuwahakikishia wateja wetu kuwa Tigo inawajali na tuna nia kubwa ya kushirikisha kwenye shikikiano zetu na huduma zetu bunifu ambazo zinahusisha na aina ya maisha yetu ya kila siku. Ningependa pia kuwahakikishia wateja wetu  kwamba  hawataingia  garama zozote za simu zaki mtandao wakati wakitumia  huduma hii  mpya ya Tigo Pesa.

Afrika sasa ni bara ya pili ulimwenguni linaloongoza katika soko  la simu za mikononi duniani, likiwa na zaidi ya watumiaji wa simu milioni 620. Zaidi ya miaka kumi iliyopita namba za miunganisho ya simu Africa imeongezeka kwa asilimia 30 kwa mwaka na inakadiriwa kufikia milioni 735 kufikia mwisho wa mwaka 2013. 


Pamoja na hilo kuwekuwa na ongezeko kubwa la mahitaji ya usafiri bora na suluhisho la usafiri pia limekuwa kwa kiwango kikubwa safari na suluhisho la usafiri bora na nafuu Afrika nzima kwa ujumla, hili limeambatana na ongezeko kubwa la kukua kwa uchumi barani Afrika.

Post a Comment

أحدث أقدم