YANGA YASHEREHESHA UBINGWA WAKE KWA KUMNYONYOA MNYAMA 2-0, NGASA ATEKWA NA MASHABIKI WA YANGA

 Wachezaji na viongozi wa Yanga wakishangilia ubingwa kwa kufungua na kuripua Champagn, baada ya kukabidhiwa Kombela lao la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Barailiyomalizika leo, ambapo Yanga imeshangilia ubingwa wake kwa kumfunga mtani wake wa Jadi Simba, mabao 2-0, katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 
Mabao ya Yanga, yalifungwa na Didier Kavumbagu, aliyeunganisha mpira kwa kichwa Kona iliyopigwa na Haruna Niyonzima, kipindi cha kwanza na Hamis Kiiza, kipindi cha pili, aliyeunganisha mpira uliorushwa na Mbuyu Twite. Simba walipoteza penati yao iliyopigwa na Mussa Mudde, waliyoipata kipindi cha kwanza baada ya Canavaro kumuangusha Ngasa katika eneo la hatari, na kufanya timu hizo zina kwenda mapumziko Yanga ikiwa mbele kwa bao 1-0.
 Wachezaji wakindellea kushangilia ubingwa wao....
Katika tukio jingine ni pale mashabiki wa Yanga, walipomvizia Ngasa baada tu ya kushuka katika jukwaa alipopanda kupokea Nishani yake na timu yake iliyopanda kupokea zawadi ya mshindi wa tatu, walimvamia na kumteka na kisha kumvisha Jezi ya Yanga na kumbeba juu juu na kuanza kuzunguka naye pembezoni mwa Mashabiki wa Yanga huku wakipiga kelele za kushangilia, hadi walipotokomea naye nje ya mageti ya kutokea uwanjani humo.

Post a Comment

أحدث أقدم