Nkomola akiwa wodini amelazwa hii leo.
Nkomola akiwa na Mchumba wake Elizabeth wakati alipohudhuria send off yake huko Same.
- Wamuibia fedha na vitu mbalimbali vya maandalizi ya harusi yake
- wapora pia samani za ndani
Afisa Habari II Wizara ya Viwanda na Biashara,Edward
Denis Nkomola amevamiwa na majambazi
usiku wa kuamkia leo, nyumbani kwake Changanyikeni Dar es Salaam na kumjeruhi
vibaya mwili.
Nkomola ni bwana harusi mtarajiwa na maandalizi
ya harusi yake yapo katika hatua za mwisho ambao ndoa yake inataraji kufungwa
Juni 15 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyo tolewa na Afisa
Habari mwenzake wa Wizara hiyo, Thom Mushi kupitia mtandao wa facebook,
inaelezwa kuwa tukio hilo lilimkuta Nkomola majira ya aa saba usiku, ambapo majambazi
wanane wakiwa na silaha mbalimbali, walivamia nyumbani kwake na wakitaka wapewe
fedha alizokusanya kwa ajili ya harusi yake.
Taarifa hiyo inasema kuwa kabla ya majambazi hao
kufanikisha adhma yao hiyo walivunja mlango wa chuma (grill) na mlango wa
kawaida wakimshambulia kwa mapanga na kumjeruhi kichwani kichwani, kumvunja mkono, kumjeruhi kwa panga pajani na kumwibia
samani za ndani, fedha na vifaa mbali mbali vya harusi.
Wiki iliyopita alitoka Wilayani Same kwenye Send
Off ya mke wake Elizabeth.
Nkomola amelazwa katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili katika kitengo cha Mifupa MOI akipatiwa matibabu na hali yake
inaendelea kusimamiwa na madaktari kwa ukaribu zaidi.
Post a Comment