Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra leo imetangaza rasmi kudhamini kwa mara nyingine tena mashindano ya ngoma za asili kwa wakazi wa kanda ya ziwa. Mashindano haya yanafanyika kwa mwaka wa nane sasa na yamekuwa na hamasa na msisimko mkubwa kwa wakazi wa maeneo hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo, Meneja Masoko wa kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Bwana Fimbo Butallah alisema kwamba lengo hasa la Bia ya Balimi Extra kudhamini mashindano haya ni kufurahi pamoja na wakazi wa kanda ya ziwa katika kusherehekea msimu huu wa mavuno. Aliendelea kusema, “Mashindano haya yanaenzi na kulinda tamaduni zetu zisipotee, yanajumuisha watu mbalimbali kukutana, kufahamiana na kufurahi kwa pamoja na hii inasaidia sana kuimarisha amani na upendo baina yetu. Amani ni nguzo muhimu sana kwa Taifa letu”.
Bwana Fimbo alifafanua kwamba kwa mwaka huu mashindano ya Ngoma yatahusisha mikoa mitano ya kanda ya ziwa. Yataanza rasmi kutimua vumbi Jumamosi hii tarehe 15 June katika mkoa wa Tabora kisha kuelekea mikoa ya Shinyanga, Kagera, Mwanza na kumalizikia mkoani Mara katika mji wa Musoma. Washindi watakaopatikana katika mikoa watashindanishwa kwa pamoja ili kumpata mshindi wa kanda. Shindano la kumpata mshindi wa kanda linategemewa kufanyika jijini Mwanza katikati ya mwezi wa saba. Tarehe rasmi za mashindano haya ni kama inavyoonekana hapa chini;
1. Mkoa wa Tabora; Jumamosi tarehe 15 June Uwanja wa Ipuli Mnadani.
2. Mkoa wa Shinyanga; Jumamosi tarehe 22 June Viwanja vya wa Shycom.
3. Mkoa wa Kagera; Jumamosi tarehe 29 June Viwanja vya Kaitaba.
4. Mkoa wa Mwanza; Jumamosi tarehe 06 July Uwanja wa CCM Kirumba.
5. Mkoa wa Musoma; Jumamosi tarehe 13 July Bwalo la Magereza.
6. Mashindano ya Kanda; Jumamosi tarehe 20 July Uwanja wa CCM Kirumba.
Bwana Fimbo alizungumzia pia zawadi za mwaka huu katika ngazi ya mikoa na ngazi ya kanda kwamba Balimi Extra imetenga zaidi ya shilingi milioni saba kama zawadi. Mpangilio wa zawadi ni kama inavyoonekana hapa chini;
ZAWADI
|
NGAZI YA MKOA
|
NGAZI YA KANDA
|
Mshindi wa Kwanza
|
600,000
|
1,100,000
|
Mshindi wa Pili
|
500,000
|
850,000
|
Mshindi wa Tatu
|
400,000
|
600,000
|
Mshindi wa Nne
|
300,000
|
500,000
|
Mshindi wa Tano hadi wa Kumi kila kikundi
|
150,000
|
250,000
|
Bwana Fimbo alimaliza kwa kuwaomba wanachi wa kanda ya ziwa wajitokeze kwa wingi kufurahi kwa pamoja waburudike na ngoma zetu za asili kutoka sehemu tofauti tofauti. Aliwashukuru sana wanywaji wa bia ya Balimi Extra kwa kuchagua bia hii na kuomba waendelee kuitumia kwani ni kupitia mchango wao ndipo pia Balimi Extra inaweza kuleta burudani kama hizi kwa ajili yao.
إرسال تعليق