BARNABA AFIWA NA MAMA YAKE MZAZI LEO HII

Mwimbaji kutoka Tanzania House of Talent (THT) Barnabas Elias maarufu kama Barnaba amefiwa na mama yake mzazi alfajiri ya leo jijini Dar es salaam. Taarifa zilizothibitishwa na rafiki wa karibu na msanii mwenzake Amini , zinasema mama yake Barnaba amefariki nyumbani kwake alfajiri ya
leo Jumamosi (June 22) kutokana na presha. Tunawaombea ndugu, jamaa wote waliofikwa na msiba huo. 

Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi...Amen

Post a Comment

أحدث أقدم