
Bibi mmoja nchini Mexico amefanikiwa kuhitimu elimu ya shule ya msingi akiwa na umri wa miaka 100.
Bibi
huyo Manuela Hernandez (pichani) ambaye alizaliwa katika jimbo la
Oaxaca mnamo mwezi Juni 1913, aliacha shule ya msingi baada ya kusoma
kwa mwaka mmoja tu na kurejea kuisaidia familia yake masikini kufanya
kazi za nyumbani.
Hata
hivyo alirejea shule kuendelea na masomo mwezi Oktoba mwaka uliopita
akiwa na miaka 99 kufuatia kushauriwa na mmoja wa wajukuu zake.

Manuela Hernandez akiwa ameshikilia cheti chake cha kuhitimu elimu ya msingi.
Hivi sasa tayari amekabidhiwa diploma yake ya elimu ya msingi katika sherehe iliyofanyika katika jimbo Mexico Kusini.
Bibi Hernandez amesema sasa ataendelea na masomo ya elimu ya sekondari.
Zaidi ya nusu ya wakazi wa jimbo la Oaxaca wenye umri wa zaidi ya miaka 15 hawajamaliza elimu ya msingi.
إرسال تعليق