CCM WILAYA YA MAKETE CHAWAVUA MADARAKA BAADHI YA VIONGOZI WAKE



 Bi Mery Mbilinyi ambaye ni diwani viti maalumu tarafa ya Lupalilo wilayani Makete ambaye kwa hivi sasa anasubiri adhabu yake kutoka CCM mkoa wa Njombe
 Aliyekuwa mwenyekiti wa CCM wilaya Makete Jasel Mwamwala ambaye amepewa onyo kali
 Katibu wa ccm wilaya ya Makete Miraji Mtaturu akitoa taarifa kwa waandishi wa habari
==========
Chama cha mapinduzi wilayani Makete  kimewavua  madaraka viongozi kadhaa wa chama hicho na wengine kupewa muda wa maangalizo  wakiwemo makatibu na wenyeviti  wa matawi  na  diwani wa viti maalumu  Bi: Mary Mbilinyi  ambaye bado anasubiri  uamuzi kutoka katika ngazi ya mkoa ya chama chama cha mapinduzi

 Akitoa taarifa kwa vyombo  vya habari   katibu wa chama cha mapinduzi   wilaya ya  Makete  Bw Miraji  Mtaturu   Alisema kuwa adhabu   hiyo  kwa viongozi hao  Imetolewa  baada ya  kujadiliwa katika kikao cha kamati ya  maadili na usalama cha chama hicho na kupitshwa  na kikao cha kamati ya siasa ya kilichofanyika hapo juzi na ndipo kuamua kutoa taarifa hiyo kwa umma kwini viongozi hao wamekuwa wakivunja sheria na taratibu za chama hicho cha siasa wilayani Makete

“Katika kikao cha kamati ya maadili na usalama  ya viongozi wa chama cha mapinduzi kilichofanyika  tarehe kumi na tatu mwezi  juni kilijadili  mienendo na tabia  za baadhi ya wananchi  na viongozi na kupitishwa na kikao cha kamati ya siasa  waliobainika kuvunja sheria waliitwa na kujibu  tuhuma zao  na sisi tukajitosheleza na kuamua kuchukua uamuzi kama  ofisi ya chama ngazi ya wilaya” alisema katibu huyo. 

Akiendelea kuongea na Vyombo vya habari katibu  Huyo Aliwataja viongozi ambao wamevuliwa madaraka kutokana na kukosa sifa ya kuwa viongozi  baada ya Kukiuka maadili  ya chama hicho  kuwa ni katibu wa tawi la Luvulunge  lililopo katika kata ya Isapulano Wilayani Makete Bw.  Festo  Chaula  na katibu wa tawi la Mago lililopo katika Kata ya Lupalilo  Bw.Creto Ngomano.

Aliwataja Viongozi  waliopewa onyo na Kupewa Muda wa angalizo la miezi sita  kuwa ni pamoja na  mwenyekiti wa kijiji cha Luvulunge Bw. Daudi Mwamkinga na kiongozi mwingine ambaye ni mwenyekiti mstaafu wa chama hicho Bw Jasel Mwamwala  na kuongeza kuwa kiongozi huyo alikiri katika kikao cha kamati hiyo na ripota wetu alipopata taarifa hii alimtafuta kwa njia ya simu naye ailikana kuwa na taarifa ya kupewa onyo na chama hicho.

Pia Katibu huyo alimtaja diwani wa viti maalumu  Katika chama cha mapinduzi wilayani Makete  Bi. Mary Mbilinyi kuwa ni miongoni mwa viongozi ambao  wamekuwa wakivunja maadili ya chama hicho  cha mapinduzi  ambaye bado anasubrli uamuzi utakaoendana na adhabu utakaotangazwa na chama hicho ngazi ya mkoa wa Njombe

Aidha aliwataka viongozi wa chama hicho kuwa makini katika utendaji wao wa kazi na kusema kuwa  chama cha mapinduzi  kina mtandao mrefu  hivyo kina uwezo mkubwa wa kuwakamata  viongozi ambao wanakiuka katiba ya chama hicho.

“Nawakubusha viongozi wa chama cha mapinduzi  kwamba chama cha mapinduzi kina mkono mrefu  kinafika hadi katika ngazi ya matawi na shina na kwamba mtu yeyote ataweza  kuukwepa mkono wa chama hichi  asiwezekurekebishwa   ni jambo lisilowezekana “ alisema katibu huyo

Akizungumzia suala la mchakato wa katiba katibu huyo aliipongeza tume hiyo kwa ufanyaji wa kazi mzuri  hadi uwasilishwaji wa rasimu hiyo ya katiba na kuwaunga mkono baadhi ya viongozi wa chama chake  katika kipengere cha kuwepo kwa maraisi watatu na kusema kuwa  kujiongezea gharama  zisizo na msingi

“Naipongeza tume ya katiba chini ya Jaji mstaafu  Warioba  kwa kazi nzuri walioifanya  hadi walipofilkia  Lakini maoni ni ya kila mtu anaweza toa na kuhusu suala la  kuwa na maraisi watatu hilo hata mimi nalipinga kwani ni kujiongezea gharama  na jambo lingine ni suala la serikali ya shirikisho  hakuna sababu ya  kuwabebesha mzigo watanzania na vyama vya siasa….."   alisema katibu huyo. 

Na James Festo

Post a Comment

أحدث أقدم