CHUO KIKUU CHA TEOFELO KISANJI HALI YAZIDI KUWA TETE KATIKA, UONGOZI WA CHUO NAO WATOA TAMKO .



Hali bado ni tete katika Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji baada ya siku moja kupita tangu Chama cha Wahadhili wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKUASA) kutangaza kutotunga mitihani ya kufungia Mhula, Uongozi wa Chuo wasimama na kukanusha Mgomo huo.
 
Akisoma Tamko la kukanusha uwepo wa Mgomo huo, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Dk. Daniel Mosses amesema Mitihani itafanyika kama ilivyopangwa kuanzia Julai Mosi Mwaka huu hadi Alhamisi ya Julai 11, Mwaka huu.
 
Hata hivyo Kaimu Mwenyekiti wa TEKUASA, Amani Sembeye,alivyopigiwa simu kuhusiana na maamuzi ya Menejiment amesema msimamo wao uko pale pale.

Ameongeza kuwa kama  kungekuwa na msimamo tofauti na walivyotoa kwa vyombo vya habari awali basi wangeitisha tena mkutano mwingine kwa ajili ya kubatilisha.

Post a Comment

Previous Post Next Post