Hitmaker Diamond Platnumz jana hakuweza kuhudhuria tuzo za Kili licha ya kushinda tuzo mbili kubwa zilizopokelewa na watu wengine kwa niaba yake. Diamond amezungumza na Bongo5 kueleza sababu iliyomsababisha ashindwe kwenda kupokea tuzo zake mwenyewe.
Amesema alishindwa kwenda kwenye kilele cha tuzo hizo kubwa nchini zilizotolewa jana kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam kwakuwa alitakiwa kwenda kwenye uzinduzi wa kinywaji kipya cha kampuni ni ya Cocacola, kiitwacho Novida uliofanyika jana usiku kwenye mgahawa wa Akemi uliopo kwenye jengo la Golden Jubelee, jijini Dar.
Amesema akiwa kama balozi wa Cocacola ilikuwa ni lazima ahudhuria uzinduzi huo. Diamond alishinda tuzo mbili ikiwemo kubwa ya msanii bora wa kiume.Msikilize zaidi hapa ambapo anawashukuru pia waliompigia kura
إرسال تعليق