FAMILIA YA LISA "LEFT EYE" LOPEZ WAUMIZWA NA KITENDO CHA TLC KUURUDIA WIMBO WA WATERFALLS


familia ya Lisa "Left eye" Lopez  (TLC) imekasirishwa na kitendo cha member wenzake waliobaki, Chilli na T-Boz kuurudia na kuweka vionjo vipya ndani ya hit single yao  "Waterfalls"  na kuamua kui- release huku nafasi ya Left Eye ikiwa imeshikiliwa na msanii wa kijapani.

Chilli (kulia) na T-Boz (kushoto), wameamua kuurudia wimbo huo uliofanya vizuri sana miaka hiyo kwa ajili ya kutoa heshima katika kufikisha miaka 20 tangu kundi hilo kuanzishwa kwa kutumia sauti za mjapani Namie Amuro badala ya sauti za Left Eye (marehem)
Dada wa marehem Left Eye anaeitwa Reigndrop anaona kama wamevunjiwa heshima kwasababu hawakujua chochote mpaka pale shabiki alipoandika kupitia kwenye mtandao.

" ingekua vizuri kama wangetutaarifu kabla ya kuwa surprised kiasi hiki" 

Regndrop pia amesema mama mzazi wa Left Eye pia ameshtushwa na kuumizwa kwasabu anaamini kuweka vocal za Left eye kwenye huo wimbo kungeheshimu kumbukumbu ya mtoto wake.
Lisa Lopes alifariki April 25, 2002, kw ajali ya gari iliyotokea Honduras

Post a Comment

أحدث أقدم