Nigeria wanasemekana kuwa katika nafasi nzuri ya kushinda mechi ya leo |
Hii leo Kenya inajiandaa kushuhudia mchuano wa kufa kupona kati ya bingwa wa Afrika Super Eagles wa Nigeria na Harambee Stars wa Kenya katika uwanja wa kimataifa wa Moi Kasarani mjini Nairobi kuanzia saa kumi jioni saa za Afrika Mashariki.
Mechi hii ni ya kundi la F ya kugombania nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la Dunia mwakani nchini Brazil.Hii ni mechi ya mkondo wa pili kwa timu hizo mbili baada ya kwenda sare ya bao moja kwa moja walipocheza kwa mkondo wa kwanza mjini Calabar Nigeria mwezi jana.
Vijana wa kocha Stephen Keshi, wanatarajiwa kuendeleza ushindi wao hii leo wakijitafutia nafasi ya kuwakilisha Afrika katika michauno ya kombe la dunia nchini Brazil
Kwa vijana wa Eagles wanaosemekana kujiandaa vyema, wanafahamu kuwa ikiwa watashindwa basi itakuwa hasara kwao kwani hawataweza kwenda Brazil.
Licha ya kwenda sare mwezi jana, Nigeria inaingia kwenye mkondo huu bila ya kushindwa mechi yoyote ya makundi kati ya kumi na sita zilizocheza hadi kufikia sasa.
Wadadisi wanasema Eagles wanaonekana kuwa katika nafasi nzuri ya kushinda.
Nao upande wa Kenya chini ya ukufunzi wa Adel Amrouche, wako taabani kuboresha matokeo yao duni yanayowaweka katika nafasi ya tatu ili kwenda Brazil.
Wanaingia kwenye mechi hii wakiwa hawaonekani kuwa katika nafasi nzuri ya kushinda.
Kenya ingali kushinda mechi yoyote ya kufuzu baada ya kwenda sare tasa dhidi ya Malawi pamoja na kwenda sare ya bao moja dhidi ya Nigeria.
Kwa matokeo, Nigeria wako mbele kwenye F wakiwa na pointi 5 wakifuatwa na Malawi wenye pointi tano pia. Namibia wana pointi tatu huku Kenya ikiwa na pointi mbili.
إرسال تعليق