Picha (panorama shot) inayoonesha kwa mbali nusu ya eneo la Faraja Centre (picha: Subi. Kwa wafuatiliaji wa aina ya camera iliyotumika kupiga picha hii na nyingine zote zilizopachikwa hapo chini, ni Sony DSC-WX9, )
HISTORIA YA KITUO CHA FARAJA
Kituo cha FARAJA HOUSE kimeanzishwa na shirika la Consolata Fathers mnamo tarehe 01.05.97. Lengo lilikuwa ni kusaidia mahitaji ya jamii hasa katika sekta ya Watoto wa Mitaani, na baada ya muda lengo likapanuliwa na kuwa Watoto wenye mazingira magumu. Ipo bodi/kamati ya mipango kwa kusaidiana kubuni maendeleo ya malezi ya watoto wote. Kamati imeweza kuwashirikisha jamaa ya watoto pamoja na viongozi wa Ustawi wa Jamii, Serikali ya ngazi mbalimbali, Walimu, na Idara mbalimbali.
Kwa ujumla kituo kina sehemu kuu nne:-
Kila sehemu ina viongozi na wahudumu wake. Lengo la kituo ni kuwalea watoto wenye mazingira magumu na vijana wengine katika mazingira mazuri kwa nia ya kuwaunganisha na jamii mapema iwezekanavyo. Kwa kutimiza lengo hili tunawatembelea jamaa zao pamoja na kuwaunganisha katika mikutano na sikukuu kwa kujadili pamoja maendeleo ya vijana. Tena kimejengwa chuo cha ufundi kwaajili ya kuwafundisha njia ya kujitegemea.
Uongozi na Wahudumu IMC: Baba P. Franco Sordella ndiye anayeshughulikia hasa mambo ya Watoto wenye mazingira magumu, P. Giulio Belotti alifanya kazi kama kiongozi na msimamizi wa Cooperative.
Nyumba ya watoto wenye mazingira magumu
Ni mahali pa kulelea watoto wenye shida. Wapo? wengi wao ni yatima, tena ni kutoka mitaani. Umri ni kutoka miaka mitano hadi 22. Kati yao wapo waliosoma seminary, secondary binafsi na za serikali, vilevile bado waliosoma chuo cha ufundi.
Wengi wana matatizo ya saikolojia kulingana na chimbuko na historia ya maisha yao.
Maana wapo walioishi kwa kuiba iba tu, baadhi waliofungwa gerezani na walioishi mitaani miaka mingi.
Shida kubwa ipo kwa watoto wenye umri wa miaka zaidi ya 12/14 ambao bado walikuwa hawajasoma au waliacha masomo kwa muda. Hawa hakika ndio walihitaji uangalizi ama matunzo ya pekee.

Padre Franco Sordella (aliyechuchumaa mbele, kushoto) na watoto wa Faraja. Aliyesimama nyuma (t-shirt nyekundu ni Mwl. Aneth, na aliyesimama kulia, blauzi ya bluu ni Subi)
Kutoka na ubovu wa jengo la shule ya kijiji pamoja na korongo ambalo mara kwa mara hujaa maji ambayo huwazuia walimu na wanafunzi kutokwenda shuleni, kituo kimefaulu kujenga shule mpya karibu na kituo kikishirikiana na serikali ya kijiji na baada ya kukamilika serikali ya kijiji ili kabidhiwa rasmi ili masomo yaweze kutolewa kwa watoto wa FARAJA HOUSE na wale wa kijijini. Bado kuna watoto wengi sana wanaoishi mitaani hapo Iringa mjini, na wengine wamezoea kuja kituoni kuomba msaada. Wengine wamefaulu kurudishwa shuleni na kusaidiwa chakula, nguo, sabuni, n.k na pia kulipiwa ada, sare za shule, viatu, na mahitaji mengine kutoka uongozi wa kituo cha Faraja House.
Mpango wa malezi: watoto wa hapa kituoni wanajitegemea katika mengi kama usafi wa mazingira, usafi wa nguo zao, kusaidia jikoni, kulima bustani na kupanda maua na miti, kulima mboga, kulima mashamba makubwa mpaka kuvuna magunia hata zaidi ya 90 ya mahindi, kufuga ng’ombe, kondoo zaidi ya 200, nguruwe kutoka wawili mpaka zaidi ya 80, na upandaji wa miti kuzunguka eneo la kituo pande karibu zote. Pia katika hili kwa sasa watoto ambao wapo sio wa umri mkubwa sana hivyo kupelekea utendaji wao wa kazi kupungua nguvu na kupata msaada mkubwa kutoka kwa wanachuo na wanakijiji, hasa katika suala la kupalilia mashamba wakati wa kilimo.
Watoto wamegawanyika katika makundi mbalimbali na katika kila kikundi kuna viongozi wao ambao huitwa makepteni. Pia wakati wa likizo na mapumziko baada ya masomo watoto huwa wanajiendeleza katika vipaji vyao hasa vya michezo mbalimbali kama, mpira wa miguu, volley-ball, calcetto, table tennis, karate, kuimba, sarakasi na upigaji wa ngoma, gita na kinanda. Tuna darasa la kompyuta ambalo hutumika kuwafundishia watoto hasa wale wenye kufanya vizuri darasani.
Walezi wa kituo hiki, waliopita ni wengi katika kujaribu kulea, lakini mlezi mkuu ni mwalimu wa shule ya Msingi na ana uzoefu wa miaka 16 katika kazi hii.
MAFANIKIO:-
Katika kipindi cha miaka 16 kituo kimeweza kutekeleza karama yake ya kuwafariji watoto wengi kutoka katika familia nyingi zenye shida mbalimbali. Hakika mazuri ni mengi, kutokana na namna watoto walivyobadilika kitabia na kupata maendeleo ya kielimu na kuweza kuishi kwa pamoja na hapo kutoa tumaini la kufaulu kuishi vizuri katika jamii yoyote watakayo kuwa. Wengi wamefaulu kuhudhuria shuleni bila taabu na kuweza kusoma, kuandika na kujiongoza bila matatizo mpaka kuweza kujitegemea. Na ifuatayo ni baadhi ya mifano hai ya watu waliolelewa katika kituo cha FarajaHouse - Mgongo:-
OBADIA O. PARABOYI [MSEMINARI]
Alipohitimu darasa la saba kutoka shule ya msingi Mgongo, alijiunga na seminari ya Consolata. Alisoma hapo tokea kidato cha kwanza mpaka cha sita. Baada ya kumaliza kidato cha sita alifanya tafakari na kuamua kuwa padre, hivyo mpaka sasa yupo katika Seminari iliyoko Afrika Kusini kwa mafunzo zaidi ya wito wake. Huko pia anaendelea kufanya vizuri na tunategemea atatimiza nia iliyoko moyoni mwake. Kwa kweli amezidi kututia moyo na kuenesha ni jinsi gani ya kufanya maamuzi na kuyasimamia vema.
MALENGA C. NDUNGURU [MWANASHERIA]
Alisoma shule ya msingi Mgongo na kufaulu kuingia sekondari. Alipohitimu kidato cha nne alikwenda Ruaha International School kwa kidato cha tano na sita. Kwa muda wa miaka miwili alifanya vizuri katika masomo ya darasani na kompyuta. Pia alifaulu kupata matokeo mazuri, na kumfanya kuweza kujiunga na shahada ya sheria katika chuo cha RUCO. Na mpaka mwaka jana aliweza kuhitimu vizuri sana. Kwa sasa anazidi kuwasaidia wadogo zake huku akijipanga kuendelea kusoma zaidi kabla hajaajiriwa ili kuanza kuyakabili maisha ya kujitegemea mwenyewe.
YOHANES .I. MTEWELE. [MWALIMU]
Alipohitimu darasa la saba kutoka shule ya msingi Mgongo, alijiunga na seminari ya Consolata. Alisoma hapo tokea kidato cha kwanza mpaka cha sita. Alipohitimu kidato cha sita alichaguliwa kujiunga na elimu ya juu katika chuo kikuu cha Dodoma, akichukuwa shahada ya ualimu. Naye aliweza kufanya vizuri katika masomo yake kwa muda wote wa miaka mitatu na sasa anafanya kazi ya kufundisha walimu katika chuo cha walimu cha Consolata kilichopo Mafinga.
EDWARD JOHN. [MWALIMU]
Alipohitimu darasa la saba kutoka shule ya msingi Mgongo, alijiunga na seminari ya Consolata. Alisoma hapo tokea kidato cha kwanza mpaka cha sita. Alipohitimu kidato cha sita aliweza kujiunga na chuo cha ualimu ngazi ya diploma katika chuo kiitwacho CAPITAL mjini Dodoma. Naye aliweza kufanya vizuri katika masomo yake kwa muda wote wa miaka miwili na sasa anafanya kazi ya kufundisha katika sekondari. Anafanya kazi katika sekondari ya Udang’u, katika mkoa wa Manyara; yenye jumla ya wanafunzi 50 na walimu 6 pamoja naye. Ndio kwanza inaanza na hao ni wanafunzi wa kidato cha kwanza tu. Kwa hakika naye ameanza maisha ya kazi na kujitegemea.
ABYSALUM NJOWOKA. [DEREVA]
Alipohitimu darasa la saba kutoka shule ya msingi Mgongo, alifaulu kujiunga na sekondari ya Same iliyoko mkoani Kilimanjaro na alikuja kumalizia elimu yake katika sedondari ya Idodi. Alipohitimu kidato cha nne, alirudi nyumbani Faraja na alifaulu kujifunza gari na kuwa dereva mzuri wa kituo chaFaraja. Vilevile kwa kuwa aliweza kujifunza na kufuzu vizuri mchezo wa karate, alikuwa mwalimu kwa vijana na watoto wengi wa Faraja. Kwa kufanya hivyo kwa muda mrefu, aliweza kuomba kujaribu maisha nje ya Faraja na mpaka sasa bado anatafuta ajira katika makampuni mbalimbali ya usafirishaji wa abiria na mizigo nje na ndani ya nchi.
ELIASA HEMED [DEREVA]
Alipohitimu darasa la saba kutoka shule ya msingi Mgongo, alifaulu kujiunga na sekondari ya Isimila iliyoko Iringa. Hakuweza kumalizia elimu yake, kwani aliacha shule akiwa kidato cha tatu. Alijaribu kufuatilia kuwa tabibu wa mifugo kwa kipindi Fulani na hakufanikiwa pia. Hapo ndipo alipoweza kujiunga na mafunzo ya udereva na mpaka sasa anaendesha maisha yake kama dereva wa daladala jijini Dar es Salaaam.
PAULO MLAWA [MWANAJESHI]
Huyu hakuweza kusoma shule ya msingi Mgongo, ila alipata mahitaji yote muhimu akiwa nyumbani kwao Ipogolo. Alipohitimu darasa la saba alifaulu kujiunga na sekondari ya Isimila iliyoko Iringa. Aliweza kuvumilia maisha ya kusoma sekondari na kuweza kufaulu kuhitimu kidato cha nne. Alijaribu maisha kidogo, na kupata mawazo ya kuwa Polisi [JKT] na aliweza pia kuendelea mbele mara tu baada ya kumaliza mafunzo ya upolisi, hakuacha damu ipoe. Hivyo ilimpelekea kwenda kwenye mafunzo ya uanajeshi [JWTZ] na sasa analitumikia taifa katika kambi ya Kunduchi iliyopo hapa Dar es salaam. Safari yake na maamuzi yake hayakuwa mepesi kwani alianza huko Kigoma, akaenda Dodoma [Makatapora], Tabora, Ruvu, tena Dodoma na mwishoe ndio akaajiriwa hapa Kunduchi alipo mpaka sasa. Katika sehemu zote alitumikia mazoezi mbalimbali siyo chini ya muda wa miezi mitatu. Na sasa anaifurahia kazi ya maamuzi yake magumu na kuyazingatia.
OMBENI J. KIHWELE [MWANACHUO]
Alipohitimu darasa la saba kutoka shule ya msingi Mgongo, alijiunga na seminari ya Mafinga. Alisoma hapo tokea kidato cha kwanza mpaka cha nne akiwa seminari . Alifanya mitihani ya kumalizia elimu yake na kuchaguliwa Kigonsera - RUVUMA, na kwa kuwa ilikuwa mbali sana na nyumban; na hali yake ya kiafya kutokuwa nzuri sana, alihamia sekondari ya Nyerere mpaka hapo alipohitimu kidato cha sita. Alipohitimu kidato cha sita alichaguliwa kujiunga na elimu ya juu katika chuo kikuu cha Mwenge [MWUCE] - Ki, akichukuwa shahada ya ualimu. Naye mpaka sasa anaendelea vema na masomo yake. Anayafurahia maisha yake kama mwanachuo na kuzidi kuwa mfano kwa wengine.
OMARY KASSIM [MPISHI]
Kijana huyu pia amesoma katika shule ya msingi Mgongo kuanzia la kwanza mpaka la saba. Alihitimu vizuri masomo yake na aliamua kwenda VETA ili kujiendeleza kielimu. Aliamua kusomea mambo ya upishi, fani ya mwaka mmoja na alifaulu vizuri. Kwa sasa anafanya kazi kama mwajiriwa katika sekondari yaSt. Joseph Lyanika; Itengule iliyoko meneo ya Mbalamaziwa, kati ya Mafinga na Makambako. Anawatumikia wanafunzi wasiopungua 120, kwani ni shule mpya kabisa na ndio kwanza ina kidato cha kwanza na cha pili tu. Anaifurahia kazi yake na anaifanya kwa bidii.
ERASTO KABOGO [MSEMINARI]
Kijana huyu alisoma shule ya msingi Kibwabwa kuanzia darasa la kwanza mpaka la saba. Akachaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mpaka cha nne katika sekondari ya J.J Mungai iliyopo Mafinga. Alisoma kwa muda wote wa miaka minne na kumaliza kwa kufanya vizuri mitihani yake. Alichaguliwa kuendelea na kidato cha tano na sita katika sekondari ya Kigonsera iliyopo mkoani Ruvuma. Huko pia alionesha bidii yake katika masomo na alifaulu. Baada ya kumaliza kidato cha sita alifanya tafakari na kuamua kuwa padre, hivyo mpaka sasa yupo katika Seminari kuu iliyopo mjini Morogoro kwa masomo ya Falsafa. Huko pia anaendelea kufanya vizuri na tunategemea atatimiza nia iliyoko moyoni mwake.
APOLINARY JOHN [MWANACHUO]
Baba ninamshukuru Mungu kwa ajili yako kwa kuweza kunipa macho ya ndani ya kujua kuwa yote uyafanyayo ni kwaajili ya sisi watoto wako. Nazidi kuona uchungu kwa uzembe niliokuwa nikiufanya tangu mtoto; maana u binadamu na uliumia kwaajili yangu na wengine. UNISAMEHE! Nakushukuru kwa kunipa mwanga na nguvu mpya ya kuweza kusimama tena na kusonga mbele, hasa katika kipindi cha mgomo wa hapa shuleni, KAMWE SITASAHAU!
Namshukuru Mungu kwani matokeo yametoka na nimechaguliwa kuendelea na masomo ya mwaka wa tatu sasa. Malengo yangu makubwa ni kuwa daktari wa watoto [PAEDIATRICIAN]; naomba uniombee na usichoke kunitia moyo. Vilevile kama una mawazo tofauti juu yangu huu ndio wakati wake, usiogope maana unaweza ukawa una mtazamo ambao ni mzuri kuliko huu nilionao mimi.
Pia kuanzia mwakani mwezi wa tatu baada tu ya kumaliza huu mwaka wa tatu tutaanza kwenda wodini [hospitalini]. Kulingana na chuo chetu kukosa hospitali ya kujifunzia [TEACHING HOSPITAL], utaratibu ni kwamba kila siku saa 11 alfajiri magari ya chuo huondoka hapa chuoni na yatatusambaza katika hospitali kuu tatu kama Amana, Temeke na Mwananyamala; mpaka mwaka wa nne tutakapo maliza, hivyo tutakuwa tumezungukia hospitali zote hizo. Kwa mwaka wa tano kuna kwenda mirembe Dodoma kwa wale wenye matatizo ya akili, Ocean roda kwaajili ya kansa na kumalizia na MOI kwaajili ya mifupa. Hivyo basi tuna mwaka huu wa tatu tu kuwa hapa chuoni kwaajili ya kujisomea sana. Na miaka miwili itakayobakia ni kwaajili ya vitendo [practical] katika sehemu mbali mbali kama nilivyo elezea hapo juu.
Wachache walioshindwa kuvumilia maisha, masomo n a kuondoka kituoni. Wapo waliondoka vizuri na wapo pia walioondoka kwa kufanya uhalifu kama kuleta ukorofi shuleni kwa walimu na wenzao na wengine kuiba fedha na kukimbia nazo. Lakini bado kituo kipo pamoja nao tena hasa wanaposhindwa na kukamatwa na polisi, wanapokuwa gerezani kituo husaidia kuwatoa na kuwapa tena moyo wa kupata mtazamo mpya wa maisha. Wengine kituo kimeweza kuwarejesha nyumbani walikotoka kwa mpango wa walezi wao.

Majengo ya Chuo cha Ufundi, Faraja Vocational Training Centre, Mgongo, Iringa
2. CHUO CHA UFUNDI - CCU
Kina lengo hasa la kuwasaidia watoto wenye shida waliosoma kituoni pamoja na vijana wengine waliomaliza darasa la VII kutoka sehemu mbalimbali. Kwa sasa kina toa fani tatu: Mekanika, Useremala na ufundi wa viatu. Katika fani zote tatu chuo kina mashine nzuri na zenye kufanya kazi bila matatizo yoyote. Na vijana wamalizapo masomo yao baada ya mwaka wa tatu, chuo huwapa vifaa vya kuanzia maisha {tool-box}. Vifaa hivyo hupewa tangu waanzapo masomo yao mpaka pale wanapomaliza huondoka navyo.
Chuo kimesajiliwa chini ya uongozi wa VETA na vijana wanaweza kufanya GRADE-TEST ya serikali hapa kituoni. Mpaka sasa chuo kimeweza kutoa wahitimu wengi na mwaka huu ni mahafali ya 13.
MAONI:-
Kulingana na utandawazi, mahitaji ya jamii na dunia kwa ujumla, chuo cha ufundi kinapaswa kuongezea mambo makuu mawili. Mafunzo yakiutendaji [practical] katika kompyuta na magari, kutengeneza na kuendesha, kama inawezekana.
Vilevile katika malezi, yafaa kuwa na wanasaikolojia, semina na ziara za kuweza kutembelea vituo vingine ili kubadilishana uzoefu kama wafanyavyo watendaji katika taasisi nyingine. Hasa kwa vijana wanapofikia balehe, kuna haja ya kuwa na semina za aina ya pekee ili waweze kujengeka, maana hapo tu ndipo panapo weka daraja kubwa la kushindwa kupata matokeo mazuri. Maana kama tunavyojua malezi ya umri wa mwaka 1 mpaka 6 ndio unaotoa mwelekeo mzima wa mtu, hivyo akishajulikana mtu tabia yake anapobalehe asikose kupewa mafunzo na wataalamu maana wanapatikana.
Unisamehe kwa kuchelewa kuimaliza kazi hii kwa wakati na kushindwa kabisa kuwaelezea Baba[wewe], Mama [ANETH] na Mtoto [TEOPHIL]. Ahsante sana, kazi njema na Mungu akubariki.
Malenga Ndunguru
Iringa.
Post a Comment