Wiki iliyopita, bodi ya Madawa na Vipodozi imeteketeza tani 27 za mchele mbovu uliopelekwa Pemba.
Mchele huu wakati unateremshwa, kama wiki tatu hivi — nilikuwepo Pemba.
Wachukuzi (makuli) walioubeba mchele huu, wanasema kuwa uanawasha mwilini wakati wanaubeba. Narudia tena: huu mchele unawasha mwilini, sasa jiulize ukifika tumboni utakuwaje??
1. Hii ndio hali ya wafanya biashara wetu wazalendo, wanaleta vyakula vibovu namna hii kuwalisha ndugu, jamaa, wazee wao n.k: kwlei haki kufanya hivi?
2. Hiyo bodi ya madawa na vopodozi – mchele huu umeteremshwa Zanzibar, bandari ya Malindi, and repacked, ukaingizwa ndani ndani ya meli ya kwenda Pemba, tuseme kweli hawakuouona au ndio ‘penyeza rupia kwenye udhia’?? Najua kuwa hawa ndio walaji wazuri hapa Zanzibar, kwao wao sasa ndio imekuwa mradi na alhamuliilah watendaji wake wote sasa ‘mambo mazuri’. Mmenifahamu ninaposema hivyo?
3. Naam — sasa msimu unawadaia au umewadia kula vyakula vobovu: Holy Month of Ramadhan upo karibu – sasa jamaa wanaleta tende mbovu (ndio iftari hiyo), basmati mbovu (eid hiyo), na kila chakula kibovu kinaletwa mwezi huu — ndio thawabu zenyewe hizo jamani. au vipi?
Mpaka nguo zinazoletwa nyengine ni mbovu, na zile bei poa, lakini hapa zinauzwa kwa bei ya kukomoana. Wafanya biashara wengine hapa Zanzibar, tunasali nao, madarsa kila kona, usiku wanasali kiyam lail na wengine hutokwa na machozi — lakini analeta na kulisha watu tende mbovu, mchele mbovu, unga mbovu na bei ya kurusha juu juu.
Nafikiri kuwa hii jamii yetu kama vile imelaaniwa, wananchi ni matatizo, na viongozi ni matatizo.
Juzi ninamsikiliza Abubakar Khamis Bakar — Waziri wa Sheria na katiba, inanisikitisha sana kuona kuwa anatetea dhulma inayofanywa na viongozi na baadhi ya wananchi kuhusu nyaraka za mali za watu, hapa kuna hadithi ndefu — sitaki kuisema udhalim unaofanywa na Bofya hapa kuhusu nyarka za mali za watu. Jamani ee tunapokwenda ni dhiraa moja tu/mwana wa ndani — warka utauwacha hapa hapa!! Katika Wizara na idara zake inayodhulumu watu, moja ni hii ya Abubakar (Wakf, pale utalia, mayatima wanalizwa) mpaka sasa watu wanaiogopa sulhu yeyote kufanywa na Wakf – tumefikia hapo Zanzibar.
Chanzo:- mzalendo.net
Post a Comment