Mwanadada mkali wa soka Iringa na mikoa ya nyanda za juu kusini Speransia Mhondele akionyesha uwezo wake kisoka |
Hapa akionyesha jinsi ya kutuliza mpira kwa gamba |
Akionyesha mbinu ya kumkabili adui kwa mpira wa angani |
Hapa akijiandaa kuondoka na mpira baada ya kuutuliza kutoka hewani |
Timu ya watuma salam mkoa wa Iringa ambayo binti Speransia ( wa pili kushoto waliosimama) alipata kuonyesha soka la uhakika jana wakati wa mchezo wa kirafikin kati ya watangazaji wa radio Furaha Fm na watuma salam mchezo uliomalizika kwa watangazaji kushinda baada ya kuigagadua timu ya watuma salam mabao 2-0
.......................................................................................
Spransia Evaristo Mhondele ni binti wa miaka 18 mkazi wa Kihesa katika manispaa ya Iringa mwenye kipaji cha hali ya juu katika mchezo wa mpira wa miguu mwenye ndoto za kuj kulipa heshima kubwa Taifa la Tanzania katika soka la wanawake .
“mimi nilihitimu masomo yangu ya sekondari mwaka 2012 katika shule ya sekondari Mlamke katika Manispaa ya Iringa na nimepata kuchaguliwa kujiunga na timu za UMISETA katika mchezo wa soka wanawake “
Nilianza kucheza mpira mwaka mwaka 2010 nikiwa katika mashindano ya UMISETA yaliyofanyika katika Ifunda kwa wilaya ya Iringa ambako nilikwenda kushiriki mchezo wa Basketi .
Baada ya kufika huku nilikuta kuna ushindani mkubwa katika mchezo huo ambao nilichaguliwa na hivyo baada ya kuchujwa wengi nikiwemo mimi katika mchezo huo ndipo nillipoamua kubadili mchezo na kuanza kucheza mchezo wa mpira wa miguu kwa kufanya mazoezi .
Nilifanya mazoezi usiku na mchana na baada ya mashindano mengine ya UMISETA ndipo nilipoamua kuelekeza nguvu huko na kujiunga kabisa katika timu ya mpira wa miguu ya wanawake .
Kujiunga kwangu na timu ya mpira wa miguu wanawake kuniliwezesha kupita hatua kwa kuchaguliwa kuwakilisha mkoa wa Iringa katika mashindano ya kanda ya kusini kwa kuelekea mkoani Ruvuma kwa mara ya kwanza kufika katika mkoa huo na baada ya kufanya vizuri huko nilichaguliwa kuwakilisha kanda ya kusini katika mashindano ya kitaifa yaliyofanyika Kibaha mkoani Pwani .
“ Jitihada binafsi nilizoonyesha na wachezaji wenzangu tuliiwezesha timu yetu kutoka kanda ya nyanda za juu kusini kushika nafasi ya tatu kitaifa “
Mchezaji huyo anadai kuwa ndoto yake kubwa katika soka kuja kuchezea timu kubwa za kitaifa ili kuweza kuonyesha uwezo wake zaidi .
“Kwa sasa nasuburi ruhusa ya mzazi wangu ili kuweza kuniruhusu kujikita zaidi katika michezo ili kuweza kutafuta fursa ya kulitumikia Taifa langu Tanzania katika michezo …..nilishindwa kujiunga na timu za wanawake nje ya mkoa kutokana na wazazi kunizuia kutokana na wakati huo nilikuwa masomoni “
Spransia anasema kuwa katika maisha yake wakati akiwa shule kwa sehemu kubwa alikuwa akiwaza michezo zaidi na hasa kuwa na ndoto ya kuja kuchezea timu kubwa za mpira wa miguu kwa wanawake na yawezekana hata kufeli kwake kulitokana na mawazo ya michezo .
Hata hivyo anasema kuwa kati ya mambo ambayo katika maisha anaona bado kufanikiwa na hana ndoto ya kukimbilia kuolewa wala katika mahusiano na wanaume kwa sasa ni kutokana na kutotimiza azma yake ya kuchezea timu kubwa ya soka wanawake nje ya mkoa wa Iringa .
Kwani amesema katika mashindano ya UMISETA kwa jitihada zake binafsi amepata kuifungia timu yake magoli matatu na kuwa kwa sasa baada ya kuhitimu elimu ya sekondari amepata kuchezea timu mbali mbali kama Kwa kilosa FC , Sengo FC na timu ya watuma salam mkoa wa Iringa wanaume ambapo kwa upande upande wa Sengo Fc nimepata kufunga magoli mawili .
Pia amesema kuwa anaomba chama cha mpira wa miguu wanawake Taifa iwapo kuna nafasi ya kusajili wachezaji wapya kuweza kumtazama hata kumpa nafasi ya majaribio ili aweze kuonyesha kipaji chake .
Mwandishi wa makala haya alipata kushuhudia kandanda safi iliyoonyeshwa na mchezaji huyo Speransia wakati wa mchezo wa kirafiki kati ya timu ya watuma salam mkoa wa Iringa na timu ya watangazaji wa kituo cha radio Furaha Fm ambapo mchezaji Speransia alipata kuchezea timu ya watuma salam na kuwa binti pekee katika timu hiyo ya wanaume ila aliweza kuwahenyesha watangazaji wa radio Furaha Fm japo ndio iliyoweza kushinda kwa magoli 2-0 dhidi ya watumasalam
Mwandishi wa makala haya ni mmiliki wa mtandao wa matukiodaima
|
إرسال تعليق