Siku chache zilizopita Uganda’s finest singer Juliana Kanyomozi aliibuka na kujibu tetesi zilizozagaa kuwa anategemea kuolewa na aliyekuwa jaji mwenzake katika shindano maarufu la kusaka vipaji Afrika Mashariki, Tusker Project fame, Jaji Ian.
Baada ya uvumi huo kuibuka Juliana mwenye miaka 31 alicheka na kuandika “Hahaha. So now I’m getting married to judge Ian!!!!! Ha abanauganda u can yap!!!” na Jaji Ian ambaye tayari ameshaoa alijibu kwa kuandika “She is worth a lot more!! will comply:-)”
Baada ya majibu hayo yaliyoonekana kutowaridhisha mashabiki wake ambao walikuwa bado wakihoji na kuamini kuwa Juliana na Ian wana mahusiano, ndipo Juliana aliamua kutoa ufafanuzi na kukanusha rasmi juu ya uvumi huo, aliandika:
“Hey friends, I’ve seen some disturbing rumours on Facebook and would like to categorically say, I’m NOT planning any wedding with judge Ian. I’ve also never had any romantic relationship with him and have no intentions to do so. Ian is someone I’ve worked with on TPF and that’s it. I have a lot of respect for him as a person, fellow judge and family man. These rumours are misrepresenting and unfair.”
Mwimbaji huyo aliyeiteka Afrika Mashariki na nyimbo zake kama Nabikoowa, Usiende Mbali aliyomshirikisha Bushoke, Haturudi Nyuma aliyomshirikisha Kidumu na zingine, ana mtoto mmoja wa kiume aliyempata na mpenzi wake wa zamani ambaye ni mfanyabiashara wa Uganda aitwaye Amon Lukwago
إرسال تعليق