Kenya kucheza COSAFA

Kikosi cha Kenya
Kikosi cha Kenya kitakachoshiriki katika mashindano ya soka ya COSAFA yatakayoandaliwa nchini Zambia mwaka huu kimetajwa.
Kocha mkuu wa Kenya Adel Amrouche ametaja kikosi cha wachezaji ishirini na wawiili wengi wao wakiwa wale walioakilisha kenya katika michuano ya hivi karibuni ya kufuzu kwa kombe dunia.
Wachezaji wawili wanaocheza soka ya kulipwa nchini Afrika Kusini, mlinda lango Brian Mandela na David Gitari wote wanaocheza soka nchini Afrika Kusini ni miongoni mwa wachezaji waliotajwa.
Kenya itakuwa ikishiriki katika mashindano hayo ya COSAFA kwa mara aya kwanza, baada ya kupata mwaliko rasmi kutoka kwa waandalizi wa mashindano hayo, fursa ambayo kocha Amrouche anasema itakuwa nzuri kwa wachezaji wake kufanya mazoezi zaidi kwa pamoja.
Harambee stars imejumuishwa katika kundi B pamoja la Lesotho, Botswana na Swaziland.
Ikiwa watafuzu kwa raundi ijayo, Kenya huenda wakacheza na Angola katika hatua ya robo fainali.
Timu hiyo ya Kenya imeratibiwa kucheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Lesotho mjini Kitwe Julai Saba mwaka huu.

Kikosi cha Kenya

Golikipa: Duncan Ochieng, Wilson Obungu, Jerim Onyango
Walinda lango: Mulinge Ndetto, David Owino, David Ochieng, Brian Mandela, Joackons Atudo

Kiungo: Mohammed Musa, John Mwangi, Edwin Wafula, Peter Opiyo, Francis Kahata, Edwin Lavatsa, Teddy Akumu, Collins Okoth
Washambulizi: Johanna Omolo, David Gateri, Jamal Mohammed, Ali Bhai, Aboid Omar, David Seda

Post a Comment

Previous Post Next Post