KIKOSI CHA ZIMA MOTO CHAZIDI KUTOA ELIMU JUU YA TAHADHARI YA MOTO

Kikosi cha zima moto kimeendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa kinga na tahadhari ya moto katika meneo mbalimbali ya makazi ya watu ikiwemo sehemu ya kuufanyia biashara.
 
Akizungumza Kamanda wa kikosi cha zimamoto mkoa wa Iringa KENEDY KOMBA, amesema kuwa lengo la kufanya hivyo ni kuondoa kero kwa wananchi ili wafahamu ni kitu gani wanalipia pamoja na manufaa yake.
 
Amesema zoezi hilo hufanyika kila mwaka wa fedha wa serikali kuanzia julai 1 mwaka husika mpaka mwaka unaofuata juni  30.
 
Aamesema kuwa mbali na kutoa elimu pia kuanzia tarehe 1 mwezi wa kumi mwaka jana walikuwa wakifanya zoezi hilo pamoja na ukusanyaji wa madhuhuri ya serikali na muda wake umekwisha na kwa wale wote watakaokuwa hawajakamilisha sheria itachukua mkondo wake.
 
Aidha amesema kuwa kwa wale ambao hawajafikiwa wafike wenyewe katika ofisi ya kamanda wa zimamoto na kwa wale ambao wamefikiwa na wamepewa hati ya malipo  wanapaswa kufahamu kuanzia sasa ndani ya siku  saba watafikishwa mahakamni.
 
Kwa upande wa wamiliki wa vyombo vya usafiri amesema kuwa kodi yao inakatwa kupitia TRA na baada ya kukatwa pesa hizo wanatakiwa kufika katika ofisi ya kamanda wa zimamoto na uokoaji ili kukaguliwa na kupewa ushauri vifaa gain vinafaa kuwekwa katika vyombo hivyo na namna ya kutumia vyombo hivyo na ili kuthibitisha kama umekaguliwa unapewa fomu maalum.

Post a Comment

أحدث أقدم