Baada ya lile shindano la kuwania Tuzo za Kilimanjaro Music Awards kumalizika vizuri sasa kama ilivyo kawaida ya kampuni ya Kilimanjaro … inakuja na Tour inayofanyika katika baadhi ya mikoa hapaTanzania …
Tour hiyo ilikuwa ikihusisha wasanii ambao hushinda Tuzo hizo na kuzunguka nao mikoani humo, lakini safari hii itaenda na wasanii waliokuwemo kwenye categories pia, yaani nominees na hadi sasa Tour hiyo imepangwa kuzunguka katika mikoa 8 ambapo Mkoa wa Dodoma ndio utakuwa mkoa wa kwanza kufanyika show ya tour hiyo ambayo inatarajiwa kufanyika tarehe 22 June …
Baadhi ya wasanii wameshathibitisha kushiriki huko na kutumbuiza siku hiyo ambao ni Joh Makini, Barnabas, Diamond Platinumz, Lady Jay Dee, Prof Jay, Roma Mkatoliki na wengineo …
Post a Comment